-
Katika upeo wa unyama, Israel imetumia silaha 'zilizoyeyusha' maelfu ya Wapalestina Ghaza
Feb 11, 2026 23:02Uchunguzi uliofanywa na televisheni ya Al Jazeera ya Qatar umefichua kuwa, utawala wa kizayuni wa Israel umetumia silaha zilizopigwa marufuku kimataifa zenye joto kupindukia katika vita vya mauaji ya kimbari huko Ghaza, na kupelekea "kuyeyuka" maelfu ya miili ya Wapalestina.
-
Hamas: Ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu mateka inathibitisha uhalifu wa Israel
Feb 11, 2026 06:02Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imesema kwamba taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa, ambayo imerekodi ukatili unaofanywa na utawala vamizi wa Israel dhidi ya mateka wa Kipalestina katika vituo na mahabusi zake, inathibitisha zaidi ukiukaji wa sheria za kimataifa ambao haujawahi kutokea unaofanywa na utawala huo.
-
Mpango wa hatua nne wa Netanyahu wa kuumeza Ukingo wa Magharibi
Feb 10, 2026 22:52Uamuzi wa baraza la mawaziri la Benjamin Netanyahu siku ya Jumapili kuhusu Ukingo wa Magharibi ulikuwa msumari wa mwisho katika jeneza la udanganyifu na matumaini ya wale waliofikiri kwamba chini ya kivuli cha makubaliano na wavamizi wa Kizayuni, inawezekana kupata haki za Wapalestina.
-
Katibu Mkuu wa UN alaani mradi mpya wa Israel wa kunyakua maeneo ya Ukingo wa Magharibi
Feb 10, 2026 03:51Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, ameonyesha wasiwasi mkubwa na kulaani uamuzi wa hivi karibuni wa Israel wa kuidhinisha hatua zinazorahisisha upanuzi wa makaazi ya walowezi wa Kizayuni na kupanua udhibiti wa kiutawala na utekelezaji wa sheria wa Israel katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa.
-
Kuungana makundi ya Kipalestina dhidi ya njama za utawala wa Kizayuni katika Ukingo wa Magharibi
Feb 09, 2026 23:03Makundi ya mapambano ya ukombozi ya Palestina yamesisitiza ulazima wa kukabiliana na mipango ya Wazayuni wenye misimamo mikali katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
-
Harakati ya BDS yalaani undumakuwili wa Human Rights Watch
Feb 09, 2026 06:39Kamati ya Kitaifa ya Palestina ya harakati inayopinga dhulma na ukandamizaji wa utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina BDS imelikosoa vikali shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch kwa kutoa ripoti za upendeleo zinazoakisi haki za Wapalestina, ikiwa ni pamoja na haki ya kurejea katika ardhi za mababu zao, na kudogosha ukiukwaji wa haki za Wapalestina wa Gaza unaofanywa na utawala wa Kizayuni.
-
Hamas yalaani mradi wa kifashisti na kikoloni wa Israel unaolenga kulitwaa eneo la Ukingo wa Magharibi
Feb 08, 2026 23:30Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imelaani vikali maamuzi mtawalia yaliyopasishwa na baraza la usalama la Israel jana Jumapili. Hamas imeyataja maamuzii hayo kuwa ni sehemu ya mradi wa kifashishti, wa kikoloni na wa kilowezi wenye lengo la kulitwaa eneo la Ukingo wa Magharibi na kuliunganisha na ardhi nyingine zilizoghusubiwa za Palestina.
-
UNICEF: Israel imeuwa watoto 37 wa Kipalestina katika mashambulizi Gaza mwaka huu
Feb 08, 2026 05:42Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF limeeleza kuwa watoto wa Kipalestinan wasiopungua 37wameuawa katika mashambuliiz ya Israel huko Gaza tangu kuanza mwaka huu wa 2026.
-
Maelfu ya Wairaqi wajiandikisha kuingia vitani kuisaidia Iran endapo itashambuliwa na Marekani
Feb 08, 2026 02:46Maelfu ya Wairaqi wamesaini hati ya ahadi ya kusaidia kuihami Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iwapo itashambuliwa kijeshi na Marekani.
-
Akademia ya Geneva: Waliofariki Ghaza wanakaribia 200,000, watu wamepungua kwa 10%
Feb 07, 2026 22:56Stuart Casey Maslen, mkuu wa Akademia ya Geneva ya Sheria za Kimataifa za Kibinadamu na Haki za Binadamu amesema, tangu Oktoba 2023 hadi sasa, idadi ya watu huko Ghaza imepungua kwa zaidi ya 10%, hali inayoashiria kutokea vifo takribani laki mbili.