-
Askari wa Israel wavamia misikiti mjini Nablus na kuzuia Swala ya Ijumaa
Mar 07, 2025 07:31Vikosi vya jeshi la Israel vimevamia misikiti kadhaa katika mji mkongwe wa Nablus, eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu, na kuzuia kuswaliwa Swala ya Ijumaa.
-
70 wauawa katika mapigano baina ya pande kinzani Syria
Mar 07, 2025 07:28Zaidi ya watu 70 wameripotiwa kuuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa nchini Syria kutokana na mapigano makali kati ya wanamgambo wa kundi la kigaidi linalotawala la Hay’at Tahrir al-Sham (HTS) na makundi ya Muqawama ya wananchi huko magharibi mwa nchi hiyo.
-
Jeshi la Israel launda kifaa cha AI cha kuwajasisi Wapalestina
Mar 07, 2025 07:27Uchunguzi mpya umefichua kuwa, kitengo cha ujasusi wa kielektroniki cha jeshi la Israel cha 8200 kimetumia mkusanyiko mkubwa wa mawasiliano yaliyonaswa kutengeneza chombo cha kijasusi cha Akili Mnemba (AI) ambacho modeli yake inashabihiana na ChatGPT, kwa lengo la kuwachunguza na kuwafanyia ujasusi wananchi wa Palestina.
-
Netanyahu awazidishia vizuizi Wapalestina vya kusali Ijumaa Msikiti wa Al-Aqsa mwezi wa Ramadhani
Mar 07, 2025 04:05Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel Benjamin Netanyahu ameidhinisha vizuizi vikali vya kuwekewa Waislamu Wapalestina kuingia katika Msikiti wa Al-Aqsa kwa ajili ya Sala ya Ijumaa wakati huu wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
-
HAMAS yasema imejiandaa 'kwa chochote kitachotokea' baada ya 'onyo la mwisho' alilotoa Trump
Mar 07, 2025 00:02Brigedi za Izzuddinul-Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS zimetangaza kwamba, zimejiandaa kwa "chochote kitachotokea" na zingali ziko kwenye hali ya "tahadhari kamili", zikisisitiza kuwa, vitisho vya utawala wa Kizayuni wa Israel vya kuanzisha tena vita dhidi ya Ukanda wa Ghaza havitatoa hakikisho kwa utawala huo dhalimu la kuweza kuwakomboa mateka wake.
-
Yemen: US kuiweka Ansarullah katika orodha ya ugaidi haina uhalali wowote
Mar 06, 2025 23:03Afisa mmoja mwandamizi wa Yemen amepuuzilia mbali hatua ya Marekani ya kuitambua Harakati ya Muqawama ya Ansarullah kama kundi la kigaidi, akisema uamuzi huo hauna uhalali wowote.
-
Hamas yajibu kimantiki bwabwaja mpya za Trump
Mar 06, 2025 06:28Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas amesema upayukaji na vitisho vya Trump vinavuruga makubaliano ya kusitisha mapigano kwani vinauchochea utawala wa Kizayuni wa Israel kutotekeleza wajibu wake.
-
Utawala wa Kizayuni wafanya njama za kudhibiti misaada inayoingia Ghaza
Mar 06, 2025 06:28Maafisa kutoka mashirika matano makubwa ya misaada duniani na Umoja wa Mataifa wameonya leo Alkhamisi asubuhi kuhusu njama za utawala wa Kizayuni wa Israel za kuchukua udhibiti wa moja kwa moja wa misaada ya kibinadamu inayoingia kwenye Ukanda wa Ghaza.
-
HAMAS yakaribisha mpango wa Waarabu wa kuijenga upya Gaza
Mar 05, 2025 22:56Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina Hamas imekaribisha mpango wa kuikarabati na kuijenga upya Gaza, uliopitishwa katika mkutano wa dharura wa viongozi wa nchi za Kiarabu mjini Cairo, Misri. Mpango huo pia unakusudia kuzuia kuondolewa Wapalestinakatika eneo hilo lililo chini ya mzingiro.
-
Amnesty yataka kuchunguzwa jinai za kivita za Israel nchini Lebanon
Mar 05, 2025 22:56Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limetoa mwito wa kufanyika uchunguzi huru juu ya mashambulizi ya utawala wa Israel dhidi ya vituo vya matibabu, magari ya dharura na wafanyakazi wa afya nchini Lebanon, na kutaja hujuma hizo kama uhalifu wa kivita.