-
Kimbunga cha al-Aqsa chamsomba Mkuu wa Majeshi ya Israel
Jan 21, 2025 23:56Mkuu wa Vikosi vya Majeshi ya Israel, Herzi Halevi ametangaza kujiuzulu kufuatia kushindwa kwake kuzima Operesheni ya Kimbunga cha al-Aqsa dhidi ya utawala huo haramu.
-
Hamas 'yajiweka sawa' baada ya Israel kufanya shambulio la kinyama Jenin
Jan 21, 2025 23:20Wanajeshi wa Israel wamewauwa shahidi Wapalestina kumi na kuwajeruhi wengine 35 katika shambulio dhidi ya mji unaokaliwa kwa mabavu wa Jenin katika eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, na kupelekea Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas kutoa wito kwa vijana wa Kipalestina kujikusanya na kujiandaa kujibu uchokozi huo wa vikosi vamizi vya Wazayuni.
-
Utawala wa Israel umetekeleza uharibifu mkubwa na wa makusudi Gaza
Jan 21, 2025 23:16Katika kipindi hiki cha kutekelezwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza na kuondoka kwa vikosi vya utawala wa Kizayuni wa Israel, maelfu ya Wapalestina wanapaswa kurejea katika. Hata hivyo hakuna nyumba za kurejea kwani Gaza imebaki na magofu tu.
-
Nyaraka zavuja kuhusu msaada wa mafuta wa Erdogan kwa utawala wa Israel
Jan 21, 2025 07:56Mbunge wa Uturuki amewasilisha picha za satalaiti na nyaraka za data za baharini katika bunge la nchi hiyo zinazothibitisha kwamba Ankara imekuwa ikitoa msaada wa mafuta kwa utawala wa Israel.
-
Upotoshaji mkubwa! Al Jazeera yaficha shukrani za msemaji wa Hamas kwa Iran
Jan 21, 2025 03:47Kitengo cha "habari za punde" cha televisheni ya Al Jazeera ya Qatar kwenye mitandao ya kijamii, katika hatua ya kushangaza, kimechuja shukrani zilizotolewa na Obaida, msemaji wa "Brigedi za Izzuddin al-Qassam," tawi la kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) kwa Iran na Yemen.
-
Hizbullah ya Lebanon: Tutaendelea kuwaunga mkono wananchi wa Palestina hadi Israel itakapoangamizwa
Jan 21, 2025 03:38Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imesisitiza katika taarifa yake kuwa itaendelea kuwasaidia na kushikama na wananchi wa Palestina hadi utawala wa Kizayuni wa Israel utakapoangamizwa.
-
Al-Houthi: Iran ilikuwa na nafasi muhimu katika ushindi wa kihistoria wa Palestina
Jan 20, 2025 23:28Katibu Mkuu wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema kuwa, kambi ya muqawama na kambi ya uungaji mkono imetoa pigo kwa adui na kwamba, Iran ilikuwa na nafasi muhimu katika kupatikana ushindi dhidi ya utawala haramu wa Israel.
-
HAMAS: Hali za afya za wafungwa wa Kipalestina zinaakisi 'unyama na ufashisti' wa Israel
Jan 20, 2025 23:04Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imesema, hali za kiafya za wafungwa wa Kipalestina walioachiliwa kutoka kwenye magereza ya Israel zinaakisi "ukatili na ufashisti" wa utawala huo wa Kizayuni.
-
Miili 10,000 ya Wapalestina inaaminika imefunikwa na vifusi, zoezi la ufukuaji limeshapata 100
Jan 20, 2025 23:03Duru za tiba za Wizara ya Afya ya Palestina katika Ukanda wa Ghaza zimeripoti kuwa miili isiyopungua 97 imegunduliwa chini ya vifusi katika maeneo tofauti ya ukanda huo katika zoezi la ufukuaji lililoanza siku ya Jumapili baada ya kutekelezwa usitishaji vita.
-
Chombo cha Kizayuni: Hamas bado inadhibiti Ukanda wa Gaza
Jan 20, 2025 07:48Chombo kimoja cha habari cha Kizayuni kimekiri kushindwa utawala huo katika vita dhidi ya Gaza na kutangaza kuwa, Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (Hamas) bado inaudhibiti Ukanda wa Gaza.