Utawala wa Kizayuni unaharibu mazingira kusini mwa Lebanon
Jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel limeanza kuharibu mazingira ya kusini mwa Lebanon kabla ya kumalizika muhula wa usitishaji vita kati ya utawala huo ghasibu na Lebanon.
Katika hatua yake mpya kichokkozi, utawala wa Kizayuni umechoma moto miti na mimea huko kusini mwa Lebanon huku ajenda yake kuu ikiwa ni kuharibu mazingira ya eneo hilo.
Israel imedai kuwa, maeneo hayo yanaweza kutumiwa kama maficho ya wanamapambano wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon.
Umesalia muda chini ya mwezi mmoja hadi kumalizika usitishaji vita wa siku 60 uliokuwa umefikiwa kati ya Hizbullah na utawala wa Kizayuni na utawala huo umekiuka usitishaji vita mara nyingi katika kipindi hicho kidogo.
Baada ya vita vya siku 66 kati ya Hizbullah ya Lebanon na Israel, pande mbili zilikubaliana kusitisha mapigano kwa siku 60. Hata hivyo utawala wa Kizayuni haukuheshimu mapatano hayo.
Inaonekana kuwa Israel umekusudia kuzidisha mapigano baada ya kumalizika usitishaji vita huo wa siku 60; na katika upande mwingine harakati ya Hizbullah pia imejiandaa kwa ajili ya siku zijazo baada ya kumalizika usitishaji vita.