-
Waisraeli waendelea kupinga hatua ya Netanyahu ya kumtimua Gallant
Nov 06, 2024 23:00Miji mbalimbali ya Israel (Palestina inayokaliwa kwa mabavu) hususan Tel Aviv iimeendelea kushuhudia maandamano makubwa ya kupinga hatua ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu ya kumfuta kazi Waziri wa Vita wa utawala huo, Yoav Gallant.
-
Kushadidi mgogoro wa Gaza kufuatia kusimamishwa shughuli za UNRWA
Nov 06, 2024 22:57Kutokana na tangazo la kusitishwa shughuli za UNRWA, taasisi za kimataifa zimeonya kuhusu uwezekano wa kuzorota zaidi hali ya maisha ya Wapalestina hususan watoto, wanawake na wagonjwa huko Ukanda wa Gaza.
-
Kikao cha "Mahakama ya Gaza" chafanyika London kuwahukumu Wazayuni
Nov 06, 2024 02:38Kundi la wanafikra, wanaharakati wa haki za binadamu, maprofesa wa vyuo vikuu na wawakilishi wa vyombo vya habari na mashirika ya kiraia limefanya kikao cha kesi ya mfano mjini London kuuhukumu utawala wa Kizayuni wa Israel kwa tuhuma za kutenda jinai dhidi ya watu wa Palestina.
-
Maji yamfika shingoni Netanyahu; amtimua waziri wa vita, maandamano yashtadi
Nov 05, 2024 23:35Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amemfuta kazi Waziri wa Vita wa utawala huo, Yoav Gallant kutokana na kushindwa kwa utawala huo wa Kizayuni kukabiliana na mrengo wa Muqawama katika Ukanda wa Gaza na Lebanon.
-
Hizbullah yawatwanga kwa makombora wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel
Nov 05, 2024 23:01Wanamuqawama wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon wamevurumisha makombora katika kambi za kijeshi mahali walipokuwa wamekusanyika wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Wanafunzi karibu elfu 12 wa Palestina wameuawa shahidi katika mashambulizi ya Israel Gaza
Nov 05, 2024 23:00Wizara ya Elimu ya Palestina imetangaza kuwa, wanafunzi karibu elfu 12 wameuawa shahidi katika mashambulizi ya utawala wa Kizayuni huko Gaza tangu kuanza vita vya mauaji ya kimbari vya Israel dhidi ya eneo hilo Oktoba 7 mwaka jana hadi sasa.
-
Wapalestina 70 wauawa shahidi katika mashambulio ya kinyama ya Israel Ghaza
Nov 05, 2024 09:22Wapalestina wasiopungua 70 wameuawa shahidi na makumi ya wengine wamejeruhiwa, akthari yao wakiwa ni wa sehemu ya kaskazini ya Ukanda wa Ghaza katika mashambulizi ya kinyama ya anga na ardhini yaliyofanywa na jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel katika eneo hilo ndani ya muda wa saa 24 zilizopita.
-
Mufti wa Oman apongeza kuchaguliwa Sheikh Qassim kuwa kiongozi wa Hizbullah
Nov 05, 2024 04:33Katika ujumbe aliouandika kwenye akaunti yake ya X, Sheikh Ahmed bin Hamad Al Khalili, Mufti wa Oman amepongeza kuchaguliwa Sjeikh Naim Qassim kuwa Katibu Mkuu mpya wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Lebanon Hizbullah.
-
Ayatullah Sistani asikitishwa na kushindwa jamii ya kimataifa kukabiliana na uchokozi wa utawala wa Kizayuni
Nov 05, 2024 04:26Marja' wa ngazi ya juu ya Mashia wa Iraq imeeleza masikitiko yake kuhusu kushindwa jamii ya kimataifa na taasisi husika katika kuzuia hujuma za kikatili za utawala wa Kizayuni dhidi ya watu wa Palestina na Lebanon.
-
Utawala wa Kizayuni wazuia kutolewa misaada kwa waliojeruhiwa kaskazini mwa Gaza
Nov 04, 2024 08:48Shirika la Ulinzi wa Raia wa Ukanda wa Gaza limetangaza hatua ya utawala katili wa Kizayuni ya kuzuia juhudi za kuwasaidia Wapalestina waliojeruhiwa kaskazini mwa Ukanda wa Gaza.