Mufti wa Oman apongeza kuchaguliwa Sheikh Qassim kuwa kiongozi wa Hizbullah
(last modified Tue, 05 Nov 2024 08:03:54 GMT )
Nov 05, 2024 08:03 UTC
  • Mufti wa Oman apongeza kuchaguliwa Sheikh Qassim kuwa kiongozi wa Hizbullah

Katika ujumbe aliouandika kwenye akaunti yake ya X, Sheikh Ahmed bin Hamad Al Khalili, Mufti wa Oman amepongeza kuchaguliwa Sjeikh Naim Qassim kuwa Katibu Mkuu mpya wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Lebanon Hizbullah.

Amesema anafurahishwa na ukweli kwamba kwamba pengo lililopatikana baada ya kuuawa shahidi Sayed Hassan Nasrallah limejazwa baada ya kuchaguliwa Sheikh Qassem.

Sheikh Al Khalili amesema mkuu huyo mpya wa Hizbullah ataendeleza njia ya shahidi Nasrallah katika kukabiliana na hujuma za kikatili za utawala wa Kizayuni dhidi ya Lebanon na mataifa mengine ya kieneo.

Vile vile ametumai kuwa Sheikh Qassim atatekeleza jukumu hilo kwa uthabiti, ushujaa na subira hadi ushindi wa mwisho na ukombozi wa ardhi za Waislamu kutoka mikononi mwa utawala ghasibu wa Israel.

Wiki iliyopita, Sheikh Qassim, ambaye alihudumu kama naibu mkuu wa Hizbullah tangu 1991, alichukua nafasi ya Shahidi  Nasrallah, ambaye aliuawa shahidi katika shambulio la kigaidi la utawala haramu wa Israel kwenye kitongoji cha Beirut mnamo Septemba 27.

Sheikh Qassim alikuwa miongoni mwa watu waliochangia pakubwa katika kuanzishwa kwa harakati za Hizbullah na Amal.