-
Sayyid wa Muqawama; Tangu alipoanza kuwaunga mkono wanyonge hadi kubeba bendera ya Mhimili wa Muqawama
Sep 28, 2024 11:52Sayyid Hassan Nasrullah, ambaye alijulikana kama sayyid wa viongozi wa ulimwengu wa Kiarabu, alipewa jina la Sayyid wa Muqawama na Ukombozi kwa sababu ya msisitizo wake juu ya kanuni na maadili yake katika kuwatetea wanaodhulumiwa na mapambano yake makali dhidi ya ubeberu.
-
Hizbullah yathibitisha: Sayyid Hassan Nasrullah ameuawa shahidi katika hujuma ya kigaidi ya Israel
Sep 28, 2024 10:26Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imethibitisha kuwa Katibu Mkuu wa harakati hiyo, Sayyid Hassan Nasrullah, amuawa shahidi katika mashambulizi makubwa ya anga ya Israel yaliyolenga majengo ya makazi ya raia kusini mwa Beirut, jana Ijumaa.
-
Guardian: Shambulio lolote la ardhini litakalofanywa na Israel dhidi ya Lebanon litafeli
Sep 28, 2024 07:50Gazeti la Guardian la Uingereza limeandika kuwa operesheni yoyote ya ardhini itakayofanywa na utawala wa Israel dhidi ya Lebanon itafeli na kugonga mwamba.
-
Vikosi vya Ulinzi vya Yemen vyazipiga makombora manowari 3 za Marekani katika Bahari ya Sham
Sep 28, 2024 06:44Msemaji wa Vikosi vya Ulinzi vya Yemen Brigedia Yahya Saree ametangaza kuwa, katika operesheni za kijeshi zilizotekelezwa na vikosi hivyo katika Bahari ya Sham, manowari tatu za mashambulizi za Marekani zimelengwa kwa makombora na ndege zisizo na rubani wakati zikiwa njiani kwenda kutoa msaada na uungaji mkono kwa adui Mzayunii.
-
Kinyume na uongo wa Netanyahu, UN yasema: Israel imezuia 90% ya misaada ya kuingizwa Ghaza
Sep 28, 2024 06:33Umoja wa Mataifa umesema, kuna changamoto kadhaa zinazokabili shughuli za ufikishaji misaada ya kibinadamu kaskazini na kusini mwa Ukanda wa Ghaza, na kubainisha kuwa 90% ya misaada hiyo iliyokuwa imeratibiwa kufikishwa kwenye maeneo hayo ama imekataliwa au kuzuiliwa hadi sasa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika mwezi huu wa Septemba.
-
Wazayuni washambulia tena vitongoji vya Beirut, Lebanon
Sep 28, 2024 04:28Ndega za kivita za utawala wa Kizayuni zinaendelea kumeshambulia kikatili mitaa ya kusini mwa Beirut, mji mkuu wa Lebanon.
-
Wapiganaji wa Kiislamu Iraq washambulia Israel kwa droni katika kuunga mkono Palestina, Lebanon
Sep 28, 2024 03:53Kundi la Muqawama wa Kiislamu nchini Iraq limetangaza kutekekleza operesheni mpya katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu na utawala Israel ya Palestina, na kushambulia ngome za kijeshi za utawala huo kwa kutumia ndege za kivita zisizo na rubani au droni kwa lengo la "kuunga mkono Palestina, Lebanon."
-
Wizara ya Afya Gaza: Israel inafukua na kuiba maiti za Wapalestina
Sep 27, 2024 22:50Wizara ya Afya ya Palestina katika Ukanda wa Gaza imeishutumu Israel kuwa "inafukua makaburi na kuiba miili," ya Wapalestina baada ya jeshi la utawala huo ghasibu kurudisha kontena lililokuwa na miili ya mashahidi 88 siku ya Jumatano iliyopita bila data yoyote au utambulisho wa miili hiyo.
-
Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina: Acheni kuipatia Israel silaha
Sep 27, 2024 22:49Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amehutubia Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, na kutoa wito wa kutoupatia silaha utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Al-Houthi: Hizbullah inabeba mzigo mkubwa kwa manufaa ya umma mzima wa Kiislamu
Sep 27, 2024 03:17Kiongozi wa harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema kuwa, vita vinavyoendelea hivi sasa baina ya Lebanon na utawala wa Kizayuni ni ushahidi wa wazi kwamba Hizbullah ina nafasi muhimu katika kuuhami umma wa Kiislamu na kubainisha kuwa, hujuma dhidi ya taifa la Lebanon ni muendelezo wa jinai za Wazayuni dhidi ya taifa la Palestina.