Wazayuni washambulia tena vitongoji vya Beirut, Lebanon
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i116862
Ndega za kivita za utawala wa Kizayuni zinaendelea kumeshambulia kikatili mitaa ya kusini mwa Beirut, mji mkuu wa Lebanon.
(last modified 2024-09-28T07:58:04+00:00 )
Sep 28, 2024 07:58 UTC

Ndega za kivita za utawala wa Kizayuni zinaendelea kumeshambulia kikatili mitaa ya kusini mwa Beirut, mji mkuu wa Lebanon.

Kwa mujibu wa shirika la habari la IRIB ndege za kivita za utawala huo wa kigaidi zimeshambulia eneo la al-Laylaki katika vitongoji vya Beirut huko Lebanon.

Vile vile, chombo kimoja cha usalama kimeiambia Al Jazeera kwamba ndege za kivita za utawala wa Israel zimerusha zaidi ya kombora moja linaloelekezwa kutokea mbali kwenye eneo hilo mjini Beirut.

Vyanzo vya habari vimeripoti kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel ulishambulia mara saba maeneo tofauti ya eneo hilo jana  Ijumaa.

Mashambulio makali ya utawala wa Kizayuni katika vitongoji vya kusini mwa Beirut

Utawala  wa Kizayuni umedai kuwa umelenga majengo ambayo Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Lebanon Hizbullah umehifadhi silaha zake humo, wakati ambapo Hizbullah imekanusha vikali madai hayo ya utawala wa Kizayuni ikisema hayana msingi wowote.
Jumatatu wiki iliyopita, jeshi la utawala dhalimu wa Kizayuni lilianza mashambulizi makali dhidi ya Lebanon katika maeneo mbalimbali ya kusini mwa Lebanon na mwenendo huo umeenezwa hadi Beirut.

Kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Lebanon, kutokana na mashambulizi makubwa na makali  ya jeshi la utawala wa Israel huko Lebanon, zaidi ya watu 700 wameuawa shahidi na zaidi ya wengine 2,600 wamejeruhiwa.