Spika Qalibaf: Iran haiombi usalama wake kutoka kwa mtu yeyote
Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amesema: "Iran haitaomba usalama wake kutoka kwa mtu yeyote hadi pale makosa ya kimahesabu ya maadui wa Iran yatakaporekebishwa.
Muhammad Baqir Qalibaf amesema kuwa, maadui wanajua kwamba njia pekee waliyonayo ni kukubali haki zetu za kisheria na kutokuwa na tamaa ya vita vya kutwisha au amani ya kutwisha ambapo Iran, iko katika nafasi ya ushindi katika vita kama kawaida na kuingia katika hatua ya kidiplomasia kwa utaratibu wa kimantiki."
Akihutubia kikao cha wazi cha Bunge leo, Spika Qalibaf amesema: Wiki iliyopita, ujumbe wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, unaowawakilisha wananchi wa Iran, ulishiriki katika Mkutano wa Wakuu wa Mabunge ya Dunia, na ninahitaji kuwasilisha ripoti kuhusu matukio na mafanikio yake.
Amefafanua kuwa: Mkutano huo ulikuwa muhimu kwa sababu ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Iran kuhudhuria mkutano rasmi katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa baada ya vita vya kujihami vya siku 12, na kuwepo kwa zaidi ya wajumbe 110 wa Bunge kutoka sehemu mbalimbali za dunia kuliongeza umuhimu wake.
Spika wa Bunge la Iran amesema: Lengo la kwanza la ujumbe wa Bunge la Iran katika mkutano huo lilikuwa kusahihisha "propaganda za vyombo vya habari" ambazo znaweza kuwa utangulizi wa adui kufanya makosa tena.
Qalibaf alibainisha: "Wakati watu wanaodhulumiwa wa Gaza wanapitia mauaji ya kimbari ya kimfumo, lengo letu la pili lilikuwa ni kupaza sauti ya kupinga ukandamizaji huu na kudai ubinadamu kutoka kwa serikali na taasisi za kimataifa."