DRC na Rwanda kuanzisha ushirikiano wa madini na kiuchumi
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i129096
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Rwanda zimefikia makubaliano ya kuwa na ushirikiano wa kiuchumi wakati wa mazungumzo yao ya kwanza tangu kutia saini mkataba wa amani.
(last modified 2025-08-03T12:36:01+00:00 )
Aug 03, 2025 12:36 UTC
  • DRC na Rwanda kuanzisha ushirikiano wa madini na kiuchumi

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Rwanda zimefikia makubaliano ya kuwa na ushirikiano wa kiuchumi wakati wa mazungumzo yao ya kwanza tangu kutia saini mkataba wa amani.

Makubaliano ya amani yaliyofikiwa mwezi Juni yalilenga kumaliza miongo kadhaa ya mzozo mashariki mwa Kongo. Makubaliano hayo yametaka kuongeza ufikiaji wake wa kwa utajiri mkubwa wa madini katika eneo hilo.

"Mfumo wa ushirikiano wa kiuchumi" ulioanzishwa siku ya Ijumaa ni sehemu muhimu ya makubaliano ya amani, imeeleza duru moja iliyoko karibu na mazungumzo hayo.

Taarifa zaidi zinasema, makubaliano ya amani yanalenga kuanzisha uwazi zaidi katika mitandao ya usambazaji wa madini muhimu kama vile coltan na lithiamu na unatarajiwa kuanza kutekelezwa mwishoni mwa mwezi Septemba.

Mashariki mwa DRC, eneo linalopakana na Rwanda lenye maliasili nyingi, lilishuhudia ongezeko jipya la ghasia mwaka huu wakati kundi lenye silaha la M23, likisaidiwa na wanajeshi wa Rwanda, lilipoteka miji muhimu ya Goma na Bukavu.

Baada ya miezi kadhaa ya usitishwaji mapigano kuvunjika, DRC na M23 walitia saini tamko la kanuni mnamo Julai 19 kuthibitisha kujitolea kwao kwa makubaliano ya kudumu ya usitishaji vita.

Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, watu 169 waliuawa mwanzoni mwa mwezi ulipita wa Julai kufuatia mashambulizi ya waasi wa M23 dhidi ya wakulima na raia huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.