-
HAMAS yaangamiza na kujeruhi wanajeshi wengine wa Israel katika mtego kabambe
Sep 02, 2024 07:33Brigedi za Izzuddin al Qassam, Tawi la Kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imeonesha namna iliyoweka mtego kabambe katika mji wa Jenin kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kuangamiza na kujeruhi wanajeshi kadhaa wa utawala wa Kizayuni.
-
Brigedi za Al-Qassam: Netanyahu amehusika na mauaji ya mateka wa Israel
Sep 02, 2024 03:47Tawi la kijeshi wa harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) limetoa ujumbe wa video ulioelekezwa kwa familia za mateka wa Israel wanaoshikiliwia huko Gaza ukisisitiza kuwa Netanyahu amehusika na mauaji ya mateka wa Israel katika eneo la Ukanda wa Gaza.
-
Netanyahu katika kinamasi cha mivutano na mizozo ya ndani
Sep 01, 2024 23:35Hali ya wasiwasi na mgogoro wa ndani ya Tel Aviv vimezidi kupamba moto kutokana na ongezeko la maandamano katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina (Israel) na kuongezeka hitilafu kati ya Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni, Benjamin Netanyahu, na wapinzani wake.
-
Netanyahu asema, atawatoa kafara mateka Waisraeli lakini jeshi la Kizayuni libaki Philadelphi
Sep 01, 2024 06:45Waziri Mkuu mshupalia vita wa utawala wa Kizayuni wa Israel Benjamin Netanyahu amemueleza waziri wake wa vita Yoav Gallant kwamba anafadhilisha jeshi la Israel libaki kwenye Ukanda wa Philadelphi (Mhimili wa Saladin) kuliko kuokoa maisha ya mateka ambao wangali wanashikiliwa katika Ukanda wa Ghaza.
-
Waisraeli 3 waangamizwa katika operesheni ya kulipiza kisasi karibu na al-Khalil
Sep 01, 2024 03:10Kwa uchache askari polisi wawili wa Israel na mlowezi mmoja wa Kizayuni wameangamizwa katika operesheni ya kulipiza kisasi karibu na mji wa al-Khalil, katika eneo la Palestina la Ukingo wa Magharibi.
-
Wazayuni wazidi "kumkalia kooni" nduli wa Ghaza
Aug 31, 2024 22:51Matokeo ya uchunguzi wa karibuni kabisa wa maoni uliofanywa na Kanali ya 12 ya televisheni ya Israel yanaonesha kuwa, walowezi wengi wa Kizayuni wanaoishi katika ardhi za Palestina zilizopachikwa jina bandia la Israel, wanachukizwa sana na kuendelea Benjamin Netanyahu kung'ang'ania kuwa waziri mkuu wa utawala huo.
-
Kushindwa utawala wa Kizayuni kukabiliana na makundi ya muqawama ya Palestina katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan
Aug 31, 2024 22:51Jeshi la utawala wa Kizayuni limeshindwa kukabiliana na makundi ya muqawama ya Palestina wakati huu ambapo Israel inaendeleza vita na hujuma zake huko Gaza na katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
-
Israel yatishia kumuua kigaidi Khalid Mashaal
Aug 31, 2024 04:32Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel ametoa vitisho kwamba utawala huo wa Kizayuni utamuua kigaidi Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Ughaibuni ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (HAMAS), Khaled Mash'al.
-
Shambulio la anga la Israel laua na kujeruhi Wapalestina wengine 34 Nuseirat na Khan Yunis
Aug 31, 2024 04:10Wapalestina wasiopungua 34 wameuawa na kujeruhiwa katika mashambulizi ya anga yaliyofanywa na jeshi la utawala haramu wa Kizayuni wa Israel katika kambi ya Nuseirat na mji wa Khan Yunis katikati na kusini mwa Ukanda wa Ghaza.
-
Jinamizi kwa Wazayuni katika medani ya vita ya kaskazini mwa Palestina
Aug 31, 2024 00:46Ingawa Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni alikusudia kupanua wigo wa vita vya utawala huo kusini mwa Lebanon ili kudhamini maslahi yake binafsi, lakini nguvu ya Hizbullah ya kuzuia mashambulizi na hasa kufanikiwa operesheni yake ya karibuni ya Arbaeen, ambayo imelenga vituo 11 vya kijeshi na kijasusi vya utawala wa Kizayuni, imempelekea kutafakari upya na kuhamishia uchokozi wake katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan kwa sasa.