-
Hali ngumu za watoto wa Gaza na bwabwaja za Wamagharibi
Aug 09, 2024 23:00Wakati Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Binadamu huko Palestina akitangaza kuwa mienendo isiyo ya kibinadamu ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya watoto wa Kipalestina ni jinai ya kivita, duru za Magharibi zinazodai kutetea haki za binadamu zinaendelea kunyamaza kimya mbele ya jinai hiyo na kukataa hata kuilaani kwa maneno tu.
-
UNICEF: Ghaza imegeuzwa makaburi ya watoto, hakuna mwisho wa mateso wanayopata
Aug 09, 2024 06:40Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Kuhudumia Watoto (UNICEF) umetangaza kuwa, Ukanda wa Ghaza umegeuzwa makaburi ya watoto wa Kipalestina na hakuna mwisho wa machungu na mateso wanayopata watoto hao.
-
Al-Houthi: Juhudi za Magharibi hazitazuia jibu la Iran kwa Israel
Aug 09, 2024 03:49Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen amesisitiza kuwa, kucheleweshwa kwa jibu la mhimili wa Muqawama na Iran dhidi ya jinai na ukatili wa utawala wa Kizayuni ni suala la kimkakati ili kutoa nafasi ya kuligeuza kuwa jibu madhubuti.
-
Palestina yaitaka ICC kumkamata Smotrich baada ya kutoa wito wa kuuawa Wapalestina mil. 2 kwa njaa
Aug 08, 2024 23:19Wizara ya Mambo ya Nje ya Palestina imeitaka Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) kutoa hati ya kukamatwa Waziri wa Fedha wa Israel, Bezalel Smotrich, kwa sababu ya wito wake wa kuwaua kwa njaa Wapalestina milioni mbili huko Gaza.
-
Madhara na uharibifu wa kinyama unaofanywa na Wazayuni katika mauaji ya kimbari ya Wapalestina
Aug 08, 2024 23:16Utawala wa Kizayuni wa Israel haujajiwekea mipaka yoyote katika mauaji ya halaiki na ya kimbari unayofanya dhidi ya wananchi wa Palestina. Askari wenyewe wa jeshi la utawala huo dhalimu wamekuwa wakikiri waziwazi na bila ya hofu kwamba wanawaua makusudi Wapalestina wasio na ulinzi wa Ukanda wa Ghaza.
-
Gazeti la Kizayuni: Kiyama kitaishukia Israel kama Iran na Hizbullah zitashambulia kwa pamoja
Aug 08, 2024 07:11Gazeti moja la Kizayuni limetangaza kuwa, kiyama kitaishukia Israel iwapo Iran na Hizbullah zitaamua kufanya mashambulio ya pamoja dhidi ya utawala wa Kizayuni.
-
Kikao cha OIC cha mjini Jeddah na majukumu ya nchi za Kiislamu
Aug 08, 2024 06:28Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC imeamua kuitisha kikao dha dharura mjini Jeddah, Saudi Arabia wakati huu ambapo Iran na kambi ya muqawama inajiandaa kutoa majibu makali kwa Israel kutokana na vitendo vya kigaidi vya utawala wa Kizayuni.
-
OIC yasema, Israel 'inabeba dhima kamili' ya mauaji ya Kiongozi wa HAMAS Ismail Haniya
Aug 08, 2024 03:02Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imeulaumu utawala wa Kizayuni wa Israel kwa shambulizi la kigaidi lililomuua Ismail Haniya, Mkuu wa Tawi la Kisiasa la Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS wiki iliyopita nchini Iran, ambayo Tehran imeapa kuyalipizia kisasi.
-
Katika miezi tisa iliyopita Yemen imeshambulia meli 170 za Marekani na Wazayuni
Aug 08, 2024 03:02Tovuti ya habari ya Yemen imetangaza katika ripoti yake kuwa katika kipindi cha miezi tisa iliyopita vikosi vya ulinzi vya nchi hiyo vimezishambulia meli 170 za Wamarekani na Wazayuni.
-
Kiwewe cha Wazayuni baada ya kuchaguliwa Yahya Sinwar kuwa mkuu mpya wa ofisi ya kisiasa ya HAMAS
Aug 07, 2024 22:53Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imemteua Yahya Sinwar kuwa Kiongozi wa Ofisi ya Kisiasa ya harakati hiyo ya muqawama, kujaza nafasi iliyoachwa wazi na hayati Ismail Haniyah.