-
Imarati yajiondoa kijeshi baada ya ndege za Saudia kushambulia mamluki wake Yemen
Dec 31, 2025 02:49Wizara ya Ulinzi ya Imarati imetangaza kwamba imeamua kujiondoa kijeshi nchini Yemen baada ya ndege za kivita za Saudia kushambulia mamluki wa Imarati kwenye bandani ya Mukalla ya Yemen.
-
2025, mwaka ulioangamiza wanajeshi wengi zaidi wa Israel
Dec 31, 2025 02:48Jeshi la Israel limetoa takwimu kuhusu kuangamizwa idadi kubwa zaidi ya wanajeshi wake mwaka huu wa 2025 unaoisha leo Jumatano na kutangaza kwamba 14% ya maangamizi hayo yametokana na vifo vya kujiua.
-
Abu Obeida; Nembo ya uvumilivu wa Wapalestina na moyo hai wa Muqawama
Dec 30, 2025 07:13Jana Jumatatu, Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas ilithibitisha kwamba msemaji wa harakati hiyo, Abu Obeida aliuawa shahidi mapema mwaka huu katika shambulio la anga la Israel.
-
Kwa mara nyingine Saudia yaishutumu Imarati kuhatarisha usalama wake wa taifa
Dec 30, 2025 07:11Wizara ya Mambo ya Nje ya Saudi Arabia imetoa taarifa kali mno leo Jumanne ikiushutumu Muungano wa Falme za Kiarabu (Imarati) kwamba unahatarisha usalama wa taifa na haki ya Saudia ya kuchukua maamuzi.
-
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Oman wasisitiza kukabiliana na vyanzo vya machafuko katika eneo
Dec 30, 2025 03:46Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, na mwenzake wa Oman, Sayyid Badr bin Hamad bin Hamood Albusaidi, wamesisitiza umuhimu wa mashauriano na uratibu endelevu kati ya nchi za Kiislamu ili kukabiliana na sababu zinazochochea mgawanyiko na machafuko katika eneo.
-
Mahabusu 100 wa Kipalestina wameuawa katika jela za Israel ndani ya miaka miwili
Dec 29, 2025 23:15Wataalamu wa Palestina wamefichua ukatili na ukandamizaji unaowakabili mahabusu na mateka wa Palestina katika magereza ya utawala wa Israel na mienendo isiyo ya kibinadamu na ukatili wa Waziri wa Usalama wa Ndani wa utawala huo dhidi ya wafungwa wa Kipalestina.
-
Mohammed Shia' al-Sudani: Iran haiingilii mambo ya ndani ya Iraq
Dec 29, 2025 06:21Waziri Mkuu wa Iraq amesisitiza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haiingilii masuala ya ndani ya nchi hiyo ya Kiarabu.
-
Muungano wa Waandishi wa Habari: Israel imewaua wanafamilia 706 wa waandishi wa habari huko Gaza
Dec 29, 2025 03:30Jeshi la Israel limewaua watu 706 kutoka familia za waandishi wa habari katika Ukanda wa Gaza tangu kuanza kwa vita vya mauaji ya kimbari mnamo Oktoba 7, 2023. Taarifa hii ni kwa kujibu wa ufuatiliaji na nyaraka za Muungano wa Waandishi wa Habari wa Palestina.
-
Kiongozi wa Yemen: Tutachukua hatua za kijeshi dhidi ya uwepo wowote wa Israel huko Somaliland
Dec 29, 2025 03:27Kiongozi wa harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema kwamba uwepo wowote wa Israel huko Somaliland utatambuliwa kama shabaha ya kijeshi, kwa sababu ni uchokozi dhidi ya Somalia na Yemen na tishio la moja kwa moja kwa usalama wa kikanda ambalo lazima likabiliwe kwa hatua madhubuti.
-
Kanali Msaudia: Imarati inafanya njama za kuigawa vipande vipande Saudi Arabia + Video
Dec 29, 2025 02:53Kanali mmoja mstaafu wa jeshi la Saudia ametoa kauli kali ambayo haijawahi kushuhudiwa dhidi ya Muungano wa Falme za Kiarabu (Imarati) akisema kuwa, nchi hiyo ni mkono wa utawala wa Kizayuni unaofanya kazi ya kuzidhoofisha na kuziangamiza nchi za Kiarabu na hasa Saudi Arabia.