-
Pango la Simba: Tutafanya operesheni nyingi zaidi dhidi ya Israel
Jul 29, 2023 06:43Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina ya Arin al Usud (Pango la Simba) imeuonya utawala wa Kizayuni wa Israel kwamba ujiandae kupokea vipigo vikali zaidi kutoka kundi hilo la mapambano.
-
Miripuko katika Haram ya Bibi Zainab SA Syria wakati wa maombolezo ya Imam Husain AS
Jul 29, 2023 06:00Juzi tarehe 27 Julai kulitokea mripuko mwingine wa kigaidi kwenye Haram ya Bibi Zainab SA mjini Damascus Syria ikiwa ni mara ya pili katika kipindi cha saa 48. Waislamu 6 waliuawa shahidi na wengine 23 kujeruhiwa kwenye shambulio hilo la kigaidi.
-
Hamas: Utawala wa Kizayuni wa Israel unataka kuibua vita vya kidini
Jul 29, 2023 04:27Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) katika mji wa Quds unaokaliwa kwa mabavu amesema kuwa mashambulizi ya Wazayuni katika Msikiti wa al Aqsa kwa mara nyingine tena yameonyesha namna adui alivyokusudia kutangaza vita vya kidini dhidi ya al Aqsa.
-
Nasrullah: Wimbi la Muqawama katika eneo lingali liko hai
Jul 28, 2023 04:36Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema katika hotuba aliyotoa usiku wa Ashura ya Imamu Hussein mjini Beirut kuwa: Tajiriba ya Muqawama nchini Lebanon imeonyesha kuwa wimbi la muqawama katika eneo lingali liko hai.
-
Jeshi la Israel lakiri lilishindwa katika operesheni ya kijeshi liliyofanya Jenin hivi karibuni
Jul 28, 2023 04:18Duru za kijeshi za Kizayuni zimekiri kushindwa operesheni ya hivi karibuni ya kijeshi iliyofanywa na jeshi la utawala haramu wa Israel dhidi ya mji wa Jenin na kambi yake ya wakimbizi.
-
Wapalestina 42 waliuawa katika uvamizi wa Israel kwenye kambi za wakimbizi mwaka 2023:
Jul 27, 2023 04:39Utawala haramu wa Israel umeongeza ukatili wake katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Quds inayokaliwa kwa mabavu na kuua Wapalestina 42 katika mashambulizi yake dhidi ya kambi za wakimbizi tangu mwanzoni mwa mwaka huu, ripoti mpya inasema.
-
Haaretz: Nasrullah alikuwa sahihi, Israel ni dhaifu kuliko nyumba ya buibui
Jul 26, 2023 22:59Gazeti la Haaretz limezungumzia hali mbaya ya kisiasa na kiuchumi inayotawala huko Israel, kukiri kwamba, mtazamo wa Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon katika kuufananishwa utawala wa Israel na nyumba ya buibui ilikuwa sahihi kabisa.
-
Upigaji kambi wa wapinzani Tel Aviv na matokeo yasiyotabirika kwa hatima ya Israel
Jul 26, 2023 22:58Licha ya ombi binafsi la Joe Biden, marafiki wa Israel ndani ya Marekani, kauli za viongozi wa upinzani wa utawala wa Kizayuni na maandamano ya umma, muungano wa mrengo wa kulia wenye misimamo ya kufurutu mpaka wa utawala haramu wa Israel umepitisha katika bunge la Knesset sehemu ya kwanza ya mswada unaojulikana kama "Mageuzi ya Mahakama".
-
Sana'a: Nchi za Kiislamu zinapaswa kuchukua hatua za kivitendo dhidi ya wanaovunjia heshima matukufu ya kidini
Jul 25, 2023 23:14Baraza la Mawaziri la Serikali ya Uokovu wa Kitaifa ya Yemen limetoa wito kwa nchi za Kiislamu kuchukua hatua za kivitendo ili kukabiliana na mashambulizi dhidi ya matukufu ya Kiislamu.
-
Imarati na Qatar katika mkondo wa kupanua mahusiano
Jul 25, 2023 08:14Amir wa Qatar amemteua Sultan Salmeen Saeed Al-Mansouri kuwa balozi wa mpya wa nchi hiyo katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).