Nasrullah: Wimbi la Muqawama katika eneo lingali liko hai
(last modified Fri, 28 Jul 2023 08:06:13 GMT )
Jul 28, 2023 08:06 UTC
  • Nasrullah: Wimbi la Muqawama katika eneo lingali liko hai

Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema katika hotuba aliyotoa usiku wa Ashura ya Imamu Hussein mjini Beirut kuwa: Tajiriba ya Muqawama nchini Lebanon imeonyesha kuwa wimbi la muqawama katika eneo lingali liko hai.

Kwa mujibu wa tovuti ya habari ya Al-Manar, katika maombolezo ya Usiku wa Ashura yaliyofanyika eneo la kusini mwa mji mkuu wa Lebanon, Beirut, Sayyid Hassan Nasrullah ameashiria mafunzo yasiyosahaulika ya moyo wa kujitolea mhanga yaliyomo kwenye chuo na njia ya fikra ya Imamu Hussein AS
) na akasema: sehemu kubwa ya migogoro inayoendelea Lebanon na duniani inahusiana na mzozo baina ya wenye nguvuu wa kupigania madaraka na uongozi.
 
Nasrullah amebainisha kuwa vita vingi vilivyotokea katika historia vilipiganwa kwa kisingizio cha kumiliki ngawira, mafuta na kuhodhi masoko na nishati; na migogoro hiyo haijawahi katu kutokea kwa madhumuni ya kusimamisha haki na uadilifu na kuleta usawa kati ya watu.

Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon ameashiria pia sababu zilizokuwa nyuma ya pazia la moto wa vita uliowashwa katika historia na akasema: waliokuwa na vipawa na satua za kisiasa, kifedha na kiuchumi siku zote wamekuwa ndio wasababishaji wa moto wa vita uliowashwa katika kipindi chote cha historia kwa ajili kudhamini maslahi yao ya kidunia.

 
Sayyid Hassan Nasrullah amepongeza pia mchango wa  familia za mashahidi wa Lebanon katika kusimama imara na kuonyesha subira katika kufuata chuo cha fikra cha Imamu Hussein AS, na akasisitiza kwa kusema: siku zote tumeshuhudia kusimama imara, kujitolea mhanga na moyo wa subira wa familia za mashahidi katika kukabiliana na maadui; na changamoto na matatizo yote haya ambayo tumeyashuhudia wakati wote wa Muqawama dhidi ya adui, yamekuwa na taathira nyingi zenye baraka katika harakati ya Muqawama kwa wingi na ubora.
 
Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesisitiza katika hotuba yake hiyo ya  Usiku wa Ashura kwamba: Lau kama Imam Hussein (AS) angetaka msaada sasa hivi, wapiganaji, kike kwa kiume, wasingemwacha peke yake, na inapasa watu wadumishe moyo wao wa imani na jihadi.../

Tags