Abdulmalik al Houthi: Nasrallah bado ni jinamizi kwa Israel
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i131338-abdulmalik_al_houthi_nasrallah_bado_ni_jinamizi_kwa_israel
Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen, Abdulmalik al-Houthi amesemam kuwa kiongozi wa muqawama wa Lebanon shahidi Sayyid Hassan Nasrallah bado ni jinamizi kwa Israel ingawa aliuawa na utawala huo mwaka mmoja uliopita.
(last modified 2025-09-28T07:03:00+00:00 )
Sep 28, 2025 07:03 UTC
  • Abdulmalik al Houthi: Nasrallah bado ni jinamizi kwa Israel

Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen, Abdulmalik al-Houthi amesemam kuwa kiongozi wa muqawama wa Lebanon shahidi Sayyid Hassan Nasrallah bado ni jinamizi kwa Israel ingawa aliuawa na utawala huo mwaka mmoja uliopita.

Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen, Abdulmalik al-Houthi ameeleza kuwa shahidi Sayyid Hasssn Nasrullah alikuwa kitisho na jinamizi kwa Wazayuni kwa zaidi ya miongo minne.

Abdul Malik al Houthi ameeleza haya jana katika hotuba aliyotoa katika marasimu ya kumbukumbu ya kuuliwa shahidi Katibu Mkuu huyo wa zamani wa Harakati ya Muqawama ya Lebanon HIzbullah. 

Abdulmalik ameongeza kusema: Baada ya Hizbullah kuibuka na ushindi dhidi ya Israel katika vita vya mwaka 2006, mradi uliokuwa umebuniwa na Marekani wa "Mashariki ya Kati Mpya" wa kubadili mazingira ya kijiipolitiki ya Mashariki ya Kati ulisambaratishwa na mashujaa wa Lebanon. 

Amesema Sayyid Hassan Nasrullah alisaidia kusitisha njama zilizokuwa zikiongozwa na Wazayuni za kueneza kushindwa miongoni mwa mataifa ya Kiislamu. 

Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema kuwa Sayyid Hassan Nasrullah alisimama kama mlimamrefu dhidi ya mradi Mpya wa Mashariki ya Kati uiotangazwa na Marekani wakati huo.