Haaretz: Nasrullah alikuwa sahihi, Israel ni dhaifu kuliko nyumba ya buibui
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i100352-haaretz_nasrullah_alikuwa_sahihi_israel_ni_dhaifu_kuliko_nyumba_ya_buibui
Gazeti la Haaretz limezungumzia hali mbaya ya kisiasa na kiuchumi inayotawala huko Israel, kukiri kwamba, mtazamo wa Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon katika kuufananishwa utawala wa Israel na nyumba ya buibui ilikuwa sahihi kabisa.
(last modified 2026-03-27T07:58:19+00:00 )
Jul 26, 2023 22:59 UTC
  • Haaretz: Nasrullah alikuwa sahihi, Israel ni dhaifu kuliko nyumba ya buibui

Gazeti la Haaretz limezungumzia hali mbaya ya kisiasa na kiuchumi inayotawala huko Israel, kukiri kwamba, mtazamo wa Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon katika kuufananishwa utawala wa Israel na nyumba ya buibui ilikuwa sahihi kabisa.

Itakumbukwa kuwa, Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon alisisitiza katika hotuba yake kuwa: Israel ambayo ina silaha za nyuklia na yenye nguvu kubwa zaidi ya anga katika eneo hili ni dhaifu sana kuliko nyumba ya buibui.

Televisheni ya Al-Mayadeen imeripoti kuwa, kutokana na kuendelea mivutano ya kisiasa na maandamano ya watu katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) dhidi ya baraza la mawaziri la Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni, gazeti la Kiebrania la Haaretz limeandika katika ripoti yake kuwa: Mtazamo wa Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon, kuhusu "nyumba ya buibui" sasa umetimia.

Gazeti la Haaretz limeongeza kuwa: Jamii ya Israeli inaporomoka. Jeshi la anga linaangamia na makamanda wa jeshi wamekiri kwamba nguvu za jeshi la Israel zinatoweka, na inatazamiwa kuwa vikosi vya jeshi vitajiunga na wimbi la maandamano ya vikosi vya akiba na kutoroka huduma ya jeshi.

Haaretz limesema katika ripoti yake kwamba: Ni jambo lililo mbali kwamba machafuko ya sasa ya ndani ya Israel yatakoma na kwamba kwa sasa tunashuhudia hitilafu kati ya vikosi vya akiba na vikosi vingine vya jeshi la Israel.