Hamas: Utawala wa Kizayuni wa Israel unataka kuibua vita vya kidini
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i100444-hamas_utawala_wa_kizayuni_wa_israel_unataka_kuibua_vita_vya_kidini
Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) katika mji wa Quds unaokaliwa kwa mabavu amesema kuwa mashambulizi ya Wazayuni katika Msikiti wa al Aqsa kwa mara nyingine tena yameonyesha namna adui alivyokusudia kutangaza vita vya kidini dhidi ya al Aqsa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 29, 2023 04:27 UTC
  • Hamas: Utawala wa Kizayuni wa Israel unataka kuibua vita vya kidini

Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) katika mji wa Quds unaokaliwa kwa mabavu amesema kuwa mashambulizi ya Wazayuni katika Msikiti wa al Aqsa kwa mara nyingine tena yameonyesha namna adui alivyokusudia kutangaza vita vya kidini dhidi ya al Aqsa.

Itamar Ben-Gvir, Waziri wa Usalama wa Ndani wa utawala wa Kizayuni juzi Alhamisi aliushambulia Msikiti wa al Aqsa akitokea upande wa  Bab al Maghariba akiambatana na kundi la walowezi wa Kizayuni kwa mnasaba wa kukumbuka kile kilichotajwa kuwa ni "Kuharibiwa Hekalu"; kisha wakatekeleza shughili za kibaguzi za Talmudi katika eneo hilo. Wawawakilishi kadhaa wa Knesset na viongozi wa serikali ya utawala wa Kizayuni wa Israel pia walijiunga katika hujuma hiyo.  

Msemaji wa Hamas katika mji wa Quds, Muhammad Hamadeh amesema: Wananchi wa Palestina hawatasalimu amri kivyovyote vile mbele ya uvamizi na mashambulizi ya utawala wa Kizayuni na walowezi wa Kiyahudi dhidi ya Msikiti wa al Aqsa. 

Muhammad Hamadeh, Msemaji wa Hamas 

Ameongeza kuwa, uvamizi wa karibuni wa Wazayuni katika Msikiti wa al Aqsa kwa mara nyingine tena umeonyesha kuwa adui amekusudia kuibua vita vya kidini.