-
HAMAS: Kufika kwa mara ya kwanza makombora ya Muqawama hadi Quds kunafikisha ujumbe kwa wazayuni
May 12, 2023 23:16Kiongozi mmoja wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS ametangaza kuwa, makombora ya Muqawama yamefika kwa mara ya kwanza Baitul Muqaddas (Jerusalem) inayokaliwa kwa mabavu na kusisitiza kuwa hatua hiyo inabeba ujumbe kwa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.
-
Hamas yakosoa kimya cha jamii ya kimataifa kuhusiana na jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel
May 12, 2023 06:33Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) amesema kimya cha jamii ya kimataifa kuhusu jinai zinazofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel huko katika Ukanda wa Gaza kinauhamasisha utawala huo ghasibu kuzididisha mashambulizi yake dhidi ya raia wasio na hatia.
-
Kuendelea mashambulizi ya kigaidi na majibu ya makundi ya mapambano ya Palestina
May 12, 2023 03:44Katika siku ya tatu ya duru mpya ya mashambulizi ya kigaidi ya Wazayuni katika Ukanda wa Gaza, Alhamisi asubuhi ndege za kivita za Israel zilishambulia jengo la makazi huko Khan Yunis, kusini mwa Ukanda wa Gaza, ambapo Wapalestina watatu akiwemo kamanda mwingine wa Brigedi ya al-Quds na ndugu yake waliuawa, na wengine kadhaa kujeruhiwa.
-
Mufti wa Oman aunga mkono majibu ya kishujaa ya wanamapambano wa Palestina
May 12, 2023 02:14Mufti Mkuu wa Oman amesema kuwa, majibu ya kishujaa ya wanamapambano wa Palestina ya kupiga kwa makombora maeneo ya Wazayuni ni majibu ya jinai za Israel dhidi ya taifa linalodhulumiwa la Palestina na amewataka Waislamu kuwa pamoja na taifa hilo linalodhulumiwa kwani mapanmbano yao yanauwakilishi umma mzima wa Kiislamu.
-
Al Mashat ataka kususiwa bidhaa za Marekani na Wazayuni
May 11, 2023 09:37Mkuu wa Baraza Kuu la Kisiasa la Yemen amezitolea wito nchi za Kiarabu na Kiislamu kususia bidhaa za Marekani na za utawala wa Kizayuni wa Israel katika kuonyesha uungaji mkono wao kwa wananchi wa Palestina, muqawama na mapambano yao.
-
Iran, Uturuki, Russia zasisitiza kuheshimiwa mamlaka ya kujitawala Syria
May 11, 2023 02:19Mawaziri wa mambo ya nje wa Iran, Uturuki, Russia na Syria wamesisitiza kulindwa mipaka na mamlaka ya kitaifa ya kujitawala Syria na kutoingiliwa masuala ya ndani ya nchi hiyo ya Kiarabu. Mawaziri hao pia wamezindua ramani ya njia ya kuboresha uhusiano uliodorora kati ya Syria na Uturuki katika mkutano katika mji mkuu wa Russia, Moscow.
-
Kuaga kwa uchungu kwa mwanamke na msichana wa Kipalestina, na kimya cha Wamagharibi mbele ya jinai ya Kizayuni
May 10, 2023 23:37Katika mashambulizi yaliyofanywa juzi na utawala wa Kizayuni wa Israel kwenye Ukanda wa Ghaza ambapo Wapalestina 15 waliuawa shahidi, zilichapishwa picha za uchungu huzuni za mwanamke na msichana mdogo wakiwaaga watu wa familia zao waliouliwa na jeshi la Israel, jambo ambalo limeumiza nyoyo na kuwatia watu simanzi na huzuni kubwa.
-
Wapalestina wavurumisha makombora Tel Aviv kulipiza kisasi jinai za Israel
May 10, 2023 09:55Makundi ya muqawama au wapigania ukombozi wa Wapalestina huko Gaza leo yamevurumisha idadi kubwa makombora kuelekea miji ya utawala wa Israel kulipiza kisasi jinai za utawala huo dhidi ya Wapalestina.
-
Jinai mpya ya baraza la mawaziri lililofeli la Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza
May 10, 2023 07:06Katika kuendeleza jinai zake, utawala wa Kizayuni wa Israel umewaua shahidi Wapalestina 13 wakiwemo makamanda watatu wa ngazi za juu wa Saraya al-Quds, tawi la kijeshi la harakati ya Jihad Islami ya Palestina katika mashambulizi kadhaa ya kigaidi kwenye maeneo ya Ukanda wa Ghaza.
-
Saudi Arabia na Syria zatangaza uamuzi wa kurejesha uhusiano wa kidiplomasia
May 10, 2023 03:07Saudi Arabia na Syria zimetangaza uamuzi wa kurejesha uhusiano wao wa kidiplomasia, baada ya kupita zaidi ya muongo mmoja tangu Riyadh ilipochukua hatua ya kuvunja uhusiano huo na kuanza kuunga mkono makundi ya kigaidi yaliyokuwa yakipambana na serikali ya Damascus.