Wapalestina wavurumisha makombora Tel Aviv kulipiza kisasi jinai za Israel
Makundi ya muqawama au wapigania ukombozi wa Wapalestina huko Gaza leo yamevurumisha idadi kubwa makombora kuelekea miji ya utawala wa Israel kulipiza kisasi jinai za utawala huo dhidi ya Wapalestina.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Israel, takriban roketi 100 zilivurumishwa kuelekea Tel Aviv na vitongoji haramu vya walowezi wa Kizayuni katika muda wa saa moja tu leo.
Mtandao wa habari wa televisheni ya al-Mayadeen umeripoti sleo Jumatano kwamba maroketi ya Wapalestina yameharibu nyumba katika mji wa Tel Aviv.
Hospitali za Israel zilmetangaza kuwa walowezi watano wamelazwa hospitalini baada ya kujeruhiwa katika hujuma hiyo ya kulipiza kisasi ya Wapalestina huku baadhi ya duru zikidokeza kuwa Wazayuni kadhaa wameuawa katika mashambulizi hayo.
Dawood Shahab, afisa wa Jihad lsami, amesema maroketi hayo yalirushwa kujibu vitendo vya uchokozi vilivyozidi vya Israel.
Mashambulizi hayo yaliyotekelezwa na wapigania ukombozi wa Palestina leo yanakuja siku moja baada ya mashambulizi ya anga ya Israel kuwaua shahidi takriban Wapalestina 17, wakiwemo makamanda watatu mashuhuri wa vuguvugu la muqawama la Palestina la Jihad Islami.
Jana Harakati ya Jihad Islami ilitoa taarifa ikitangaza kuwa, adui Mzayuni ndiye anayehusika kikamilifu na mauaji hayo ya kigaidi na kueleza kuwa, adui hatafikia malengo yake kwa jinai hiyo.
Jihad Islami imesisitiza kuwa Saraya Al-Quds, tawi la kijeshi la harakati hiyo, pamoja na mirengo mingine ya muqawama, kamwe haitazembea katika kulipiza kisasi cha damu safi ya mashahidi hao.
Aidha harakati ya mapambano ya Arin al Usud, yenye makao yake mjini Nablus imesema katika taarifa yake ya Jumanne kwamba, "Mara hii milango ya Jahanamu itafunguliwa kwa Wazayuni kwa jinai yao hiyo.