-
Mufti wa Oman aitaka Muscat ifikirie upya uamuzi wa kuruhusu anga yake kutumiwa na ndege za Israel
Feb 26, 2023 04:23Mufti wa Oman Shekhe Ahmed bin Hamad al-Khalili ameitaka serikali ya Muscat iangalie upya uamuzi wake wa kuruhusu anga yake kutumiwa na ndege za utawala haramu wa Israel.
-
Ujumbe wa Muungano wa Mabunge ya Kiarabu wawasili Damascus, Syria
Feb 26, 2023 03:03Muungano wa Mabunge ya Kiarabu sambamba na kuunga mkono kurejeshewa nafasi yake Syria iliyokuwa nayo katika mataifa ya Kiarabu imesema kuwa, ujumbe wa muungano huo umeelekea nchini Syria.
-
HAMAS: Taifa la Palestina halitasalimu amri; jinai za Israel hazitabakia bila majibu
Feb 25, 2023 09:25Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) imesisitiza kuwa, jinai za utawala ghasibu wa Israel zitajibiwa na wanamapambano shupavu wa Kipalestina na katu hazibakia hivi hivi bila ya majibu.
-
Umoja wa Mataifa: Ujenzi wa vitongozi vya walowezi wa Kizayuni ni kinyume cha sheria
Feb 25, 2023 08:29Msemaji wa Umoja wa Mataifa ametangaza kuwa, ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni unaofanywa na Israel hauna mashiko ya kisheria na kwamba, ni ukiukaji wa wazi kabisa wa sheria za kimataifa.
-
Spika wa Bunge la Iraq ataka Syria irejeshwe katika nafasi yake katika mataifa ya Kiarabu
Feb 25, 2023 08:17Spika wa Bunge la Iraq ametoa mwito wa nchi ya Syria kurejeshwa katika nafasi iliyokuwa nayo miongoni mwa mataifa ya Kiarabu.
-
Katibu Mkuu wa Jihadul-Islami: Damu ya Mashahidi itailetea ushindi Palestina
Feb 25, 2023 03:39Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihadul-Islami ya Palestina amepongeza mchango wa kijihadi wa Mashahidi wa ardhi hiyo katika kukabiliana na adui Mzayuni na akasema, damu za Mashahidi hao ndizo zitakazoiletea ushindi Palestina.
-
Onyo la Ismail Hania kwa Israel kuhusu matokeo mabaya ya kuendelea vitendo vya utumiaji mabavu
Feb 24, 2023 23:13Ismail Hania, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) amewapongeza wananchi wa Palestina kwa kuendelea kusimama imara na kutangaza kuwa, vita na adui Mzayuni vimeingia katika awamu mpya.
-
Haniyeh: Vita na adui Mzayuni vimeingia katika hatua mpya
Feb 24, 2023 09:31Mkuu wa Idara ya Siasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) amewapongeza wananchi wa Palestina kwa kuendelea kusimama imara na kutangaza kuwa, vita na adui Mzayuni vimeingia katika awamu mpya.
-
Oman yaruhusu ndege za Israel zitumie anga yake
Feb 23, 2023 23:36Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel amedai kuwa, Oman imeidhinisha ndege za utawala huo haramu kuruka katika anga ya nchi hiyo ya Ghuba ya Uajemi.
-
Wataalamu: Netanyahu 'hana ubavu' wa kukabiliana na wanamapambano wa Palestina
Feb 23, 2023 06:38Wataalamu mbalimbali wa kijeshi wa Israel wametoa maneno makali ya kumlaumu waziri mkuu mwenye misimamo ya kufurutu ada, Benjamin Netanyahu na kusema kuwa, hana uwezo wa kukabiliana na mashambulio ya makombora ya wanamapambano wa Palestina.