Oman yaruhusu ndege za Israel zitumie anga yake
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i94386-oman_yaruhusu_ndege_za_israel_zitumie_anga_yake
Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel amedai kuwa, Oman imeidhinisha ndege za utawala huo haramu kuruka katika anga ya nchi hiyo ya Ghuba ya Uajemi.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Feb 24, 2023 03:06 UTC
  • Oman yaruhusu ndege za Israel zitumie anga yake

Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel amedai kuwa, Oman imeidhinisha ndege za utawala huo haramu kuruka katika anga ya nchi hiyo ya Ghuba ya Uajemi.

Eli Cohen amesema uamuzi huo ni mkubwa na wa kihistoria kwa uchumi na wasafiri wa utawala wa Kizayuni wa Israel. Cohen ameeleza bayana kuwa, Marekani imekuwa na mchango mkubwa katika kufikiwa uamuzi huo.

Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Oman bila kuitaja Israel kwa njia ya moja kwa moja, imeandika katika ukurasa wake wa Twitter kuwa, anga ya nchi hiyo ya Kiarabu ipo wazi kwa ndege zote ambazo zimetimiza masharti na vigezo ilivyoweka.

Hii ni katika hali ambayo, Aprili mwaka jana 2022, Oman ilikataa kuidhinisha ndege za utawala wa haramu wa Israel kuruka katika anga yake, ikionekana kujiepusha kufuata nyayo za Saudi Arabia za kujikurubisha wazi wazi kwa utawala huo pandikizi.

Hii ni baada ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Saudia (GACA) kusema katika taarifa kwamba, anga ya nchi hiyo sasa iko wazi kwa mashirika yote ya ndege, ikiwa ni pamoja na yale ya Israel, kufuatia safari ya Rais wa Marekani Joe Biden katika ufalme huo.

Maandamano ya kupinga uhusiano na Israel huko Sudan

Utawala haramu wa Israel umeongeza juhudi zake zinazoungwa mkono na Marekani za kuanzisha uhusiano wa wazi na wa kawaida na Oman, miongoni mwa nchi nyingine za Kiarabu za Ghuba ya Uajemi.

Kwa muda mrefu sasa, Oman imekuwa ikisisitiza kuwa, haitakuwa na uhusiano wa kawaida na wa wazi na Israel hadi pale suala la Palestina litatatuliwa.