Haniyeh: Vita na adui Mzayuni vimeingia katika hatua mpya
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i94406-haniyeh_vita_na_adui_mzayuni_vimeingia_katika_hatua_mpya
Mkuu wa Idara ya Siasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) amewapongeza wananchi wa Palestina kwa kuendelea kusimama imara na kutangaza kuwa, vita na adui Mzayuni vimeingia katika awamu mpya.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 24, 2023 09:31 UTC
  • Ismail Haniyeh
    Ismail Haniyeh

Mkuu wa Idara ya Siasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) amewapongeza wananchi wa Palestina kwa kuendelea kusimama imara na kutangaza kuwa, vita na adui Mzayuni vimeingia katika awamu mpya.

Ismail Haniyeh amesema katika taarifa yake ya leo Ijumaa kwamba: "Kwa heshima kamili na taadhima, tunathamini mahudhurio mkubwa ya Wapalestina katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na maeneo yote ambako wamepaza sauti ya kupigania haki."

Taarifa hiyo imetolewa baada ya maelfu ya Wapalestina katika maeneo tofauti kuitikia wito wa kundi la mapambano ya ukombozi la "Arin al-Asud" na kujitokea kwa wingi barabarani ili kuunga mkono muqawama na mapambano dhidi ya Israel na kulaani jinai za utawala wa Kizayuni huko Nablus.

Haniyeh ameongeza kuwa vita dhidi ya adui Mzayuni vimeingia katika hatua mpya na madhubuti kiasi kwamba itawaangamiza wavamizi na kuwafukuza kutoka katika ardhi ya Palestina.

Ismail Haniyeh 

Amesema, taifa la Palestina na mapambano yake ya kishujaa kamwe halitaruhusu mtu yeyote kuzima intifada inayoongezeka katika Ukingo wa Magharibi.

Mkuu wa Idara ya Siasa ya Hamas amesisitiza kuwa haya ni mapinduzi yaliyoanzia mitaani, na kila mtu huru anayepigania haki atayakubali ili kizazi cha ushindi kipeperushe bendera juu ya minara ya Al- Quds, kuba za Msikiti wa Al-Aqsa na sehemu zote tukufu za Kiislamu na Kikristo.