-
HAMAS: Tuko tayari kukabidhi uendeshaji wa Ghaza kwa kamati ya shakhsia wa kujitegemea
Jan 09, 2026 23:04Msemaji wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema, harakati hiyo ilishaamua tokea huko nyuma kwamba haitakuwa na ushiriki wa moja kwa moja katika hatua yoyote ya upangaji wa masuala ya kiidara na kiuendeshaji ya siku za usoni katika Ukanda wa Ghaza.
-
UNRWA: Misaada inayoingia Gaza inakabiliwa na vivingiti shadidi vya Israel
Jan 09, 2026 07:30Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Wakimbizi Wapalestina (UNRWA) limetangaza kuwa vizingiti vilivyowekwa na jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel katika njia za kuingia Ukanda wa Gaza vimesababisha kupungua kwa kiwango kikubwa misaada kwa Wapalestina katika eneo hilo.
-
Wizara ya Afya ya Palestina: Waliouawa shahidi Gaza ni zaidi ya 71,300
Jan 09, 2026 02:53Wizara ya Afya ya Palestina imeeleza katika takwimu zake za hivi karibuni kwamba, Wapalestina zaidi ya 71,000 wameuawa shahidi katika vita vya mauaji ya kimbari vilivyoanzishwa na utawala wa kizayuni wa Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza Oktoba 2023.
-
Utafiti: Takriban asilimia 90 ya watu katika nchi za Kiarabu wanapinga kuanzishwa uhusiano na Israel
Jan 08, 2026 22:52Idadi kubwa ya watu katika Ulimwengu wa Kiarabu wanapinga kuitambua Israel na kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala huo ghasibu. Hii ni kwa mujibu wa uchunguzi mpya wa maoni wa kikanda.
-
UN yaitaka Israel ikomeshe 'mfumo wa ubaguzi wa apathaidi' inaoendesha Ukingo wa Magharibi
Jan 07, 2026 23:35Umoja wa Mataifa kupitia Kamishna wake Mkuu wa Haki za Binadamu umesema, hatua za miongo kadhaa za Israel za kuwatenga na kuwabagua Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi inaoukalia kwa mabavu zinazidi kuongezeka, na kwa sababu hiyo umetoa wito wa kuutaka utawala huo ukomeshe "mfumo wake wa ubaguzi wa rangi wa apathaidi".
-
UAE yatuhumiwa tena na Saudia; mara hii ni kuwaunga mkono Wadruze ili kuigawanya Syria
Jan 07, 2026 23:33Televisheni ya CNN ya Marekani imeripoti kuwa, Saudi Arabia imetoa tuhuma zisizo za kawaida dhidi ya Muungano wa Falme za Kiarabu, Imarati huku kukiwa tayari kuna mvutano unaoongezeka kati ya mataifa hayo mawili ya Ghuba ya Uajemi, tuhuma ambazo zinahusu wasiwasi kuhusu namna UAE inavyojihusisha na masuala ya Syria.
-
Imarati inapanga kuijengea Israel kambi ya jeshi karibu na Saudi Arabia
Jan 07, 2026 06:43Vyombo vya habari vya Saudi Arabia vimefichua mpango wa Umoja wa Falme za Kiarabu wa kujenga kambi ya kijeshi ya Israel karibu na mpaka wa nchi hizi mbili za Kiarabu.
-
Waziri wa Ulinzi wa Pakistan: Netanyahu ni mtenda jinai anayechukiwa zaidi katika historia
Jan 07, 2026 04:07Waziri wa Ulinzi wa Pakistan amemtaja Waziri Mkuu wa Israel kuwa mtenda jinai anayechukiwa zaidi katika historia na kusema: "Uongo wa Benjamin Netanyahu dhidi ya miradi ya nyuklia ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inayoendeshwa kwa malengo ya amani ulikuwa kisingizio tu cha kuhalalisha mashambulizi ya Israel dhidi ya Iran.
-
Wazayuni wamefanya mashambulizi 24,000 katika Ukingo wa Magharibi
Jan 06, 2026 23:26Ripoti ya kila mwaka ya shirika moja la Palestina imefichua kuwa, katika kipindi cha mwaka uliopita wa 2025, Wazayuni wamefanya karibu mashambulizi 24,000 katika eneo la Ukingo wa Magharibi la Mto Jordan huko Palestina.
-
Israel yafanya mashambulizi makubwa ya anga dhidi ya Lebanon
Jan 06, 2026 08:40Israel imefanya mfululizo wa mashambulizi ya anga katika maeneo yote ya kusini na mashariki mwa Lebanon, ikiendelea kukanyaga makubaliano ya kusitisha mapigano ambayo lengo lake ni kukomesha uchokozi wa Israeli dhidi ya uhuru wa kujitawala nchi hiyo ya Kiarabu.