-
Waislamu laki moja na 50,000 wakusanyika Msikiti wa al Aqsa Palestina kuilaani Israel
Apr 23, 2022 02:57Makumi ya maelfu ya Waislamu wa Palestina walikusanyika kwenye Msikiti wa al Aqsa baada ya kutekeleza ibada tukufu ya Sala ya Ijumaa, jana na kupiga nara za kulaani jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Kukosolewa kikao cha mawaziri wa nje wa Jumuiya ya nchi za Kiarabu, kinachodai kutetea Quds Tukufu
Apr 22, 2022 22:04Katika kikao kilichofanyika Alkhamisi tarehe 21 Aprili huko Jordan, Kamati ya Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Kiarabu ambayo imepewa jukumu la kukabiliana na hatua zisizo za kisheria za utawala wa kigaidi wa Israel huko Quds Tukufu, imesisitiza udharura wa kusimamishwa mara moja uchokozi na hujuma ya Wazayuni huko Quds na katika Msikiti wa al-Aqsa.
-
Faisal Miqdad: Marekani na nchi za Magharibi zinafanya njama za kuangamiza suala la Palestina
Apr 22, 2022 02:40Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria amesema kuwa, nchi za Magharibi zinaendelea kula njama za kuvuruga na kuharibu kadhia ya ukombozi wa Palestina na haki thabiti za watu wake, hususan haki ya wakimbizi wa Kipalestina kurejea katika nchi yao na kuongeza kuwa, Damascus inafuatilia kwa wasiwas matukio hatari yanayojiri huko Quds ( Jerusalem) inayokaliwa kwa mabavu.
-
Serikali ya mseto ya Bennett na Lapid katika ncha ya kusambaratika
Apr 21, 2022 21:30Makundi ya Waarabu ndani ya serikali ya sasa ya Tel Aviv yaani United Arab List (UAL) chama kinachowawakilisha Waarabu wanaoishi ndani ya maeneo yaliyotwaliwa na Israel chini ya uenyekiti wa Mansour Abbas mbunge wa Kiarabu ambaye pia ni mwakilishi wa muungano wa serikali ya mseto ya Israel, yametoa masharti kwa ajili ya kubakia katika baraza la mawaziri la Naftali Bennett.
-
Mufti wa Oman awakosoa viongozi wa Kiarabu wanaofuturu na Wazayuni huku al Aqsa ikitiwa najisi
Apr 20, 2022 22:19Mufti Mkuu wa Oman, Sheikh Ahmed bin Hamad al-Khalili, amepongeza misimamo ya kishujaa ya wanamapambano wanaoendelea kukabiliana na uvamizi wa mara kwa mara wa Israel katika Msikiti wa Al-Aqsa katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.
-
Amnesty International: Vitendo vya Israel dhidi ya Palestina ni "uhalifu dhidi ya ubinadamu."
Apr 20, 2022 22:18Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limeitaja Israel kuwa ni utawala wa kibaguzi na kutangaza kuwa, mauaji na mateso yanayofanywa na utawala huo dhidi ya Wapalestina na kuwanyimwa haki zao ni uhalifu na jinai dhidi ya binadamu.
-
UAE, Bahrain na Saudia zinahasimiana na kila anayepinga Israel
Apr 20, 2022 06:34Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen anasema Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Bahrain na Saudi Arabia zinahasimiana na kila ambaye ni adui wa utawala haramu wa Israel na kuongeza kuwa madola hayo matatu hayataki uthabiti wa Waislamu duniani na daima yanatekeleza njama chafu.
-
Kuendelea hatua za Imarati dhidi ya taifa la Palestina
Apr 20, 2022 03:30Ikiwa ni katika kuendeleza hatua zake dhidi ya taifa la Palestina na katika kivuli cha kudumushwa vitendo vya mabavu vya utawala haramu wa Israel dhidi ya Wapalestina, serikali ya Umoja wa Falme za Kiarabu yaani Imarati, imechukua hatua nyingine mbili katika kuimarisha uhusiano wake na utawala huo wa kibaguzi.
-
Jihad al Islami: Adui Mzayuni anataka kuzusha vita vya kidini
Apr 20, 2022 03:18Kiongozi mmoja wa ngazi za juu wa harakati ya Jihad al Islami ya Palestina amesema kuwa, adui Mzayuni anafanya njama za kuzusha vita vya kidini katika eneo hili.
-
Hizbullah yataka kunzishwe harakati kubwa ya kulaani kitendo cha kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu, Sweden
Apr 19, 2022 03:46harakati ya Hizbullah ya Lebanon imetoa wito kwa Umma mzima wa Kiislamu kuanzisha harakati kubwa zaidi dhidi ya kitendo cha kuvunjiwa heshima Qur'ani nchini Sweden.