Jihad al Islami: Adui Mzayuni anataka kuzusha vita vya kidini
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i82710-jihad_al_islami_adui_mzayuni_anataka_kuzusha_vita_vya_kidini
Kiongozi mmoja wa ngazi za juu wa harakati ya Jihad al Islami ya Palestina amesema kuwa, adui Mzayuni anafanya njama za kuzusha vita vya kidini katika eneo hili.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 20, 2022 03:18 UTC
  • Kiwewe kinamfanya adui Mzayuni kutumia magari ya kijeshi kukabiliana na vijana wa Kipalestina wenye mawe tu mikononi
    Kiwewe kinamfanya adui Mzayuni kutumia magari ya kijeshi kukabiliana na vijana wa Kipalestina wenye mawe tu mikononi

Kiongozi mmoja wa ngazi za juu wa harakati ya Jihad al Islami ya Palestina amesema kuwa, adui Mzayuni anafanya njama za kuzusha vita vya kidini katika eneo hili.

Shirika la habari la Shehab la Palestina limemnukuu Daud Shahab, mmoja wa viongozi waandamizi wa Jihad al Islami akisema kuwa, vita dhidi ya wakazi wa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan huko Palestina vinazidi kuwaka moto.

Maeneo hayo hasa mji wa Jenin imekumbwa na mashambulio na uvamizi mkubwa wa Wazayuni katika maeneo ya Wapalestina kiasi kwamba hadi hivi sasa Wapalestina kadhaa wameshapigwa risasi na kuuliwa shahidi na wanajeshi makatili wa Israel tangu mwanzoni mwa mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.

Ukombozi wa Palestina umo ndani ya damu za Wapalestina hakuna tofauti baina ya wanawake na wanaume wala wakubwa kwa wadogo wala vijana kwa wazee

 

Daud Shahab ameongeza kuwa, uvamizi unaofanywa na wanajeshi madhalimu wa Israel dhidi ya wananchi wa Palestina walioko kwenye saumu ya Ramadhani hauishi kwenye eneo moja kwani utawala wa Kizayuni ni adui wa kila Mpalestina.

Kiongozi huyo wa ngazi za juu wa harakati ya Jihad al Islami vile vile amesisitiza kuwa, wananchi wa Palestina hawana chaguo jingine isipokuwa muqawama na kusimama imara kupambana na jinai na uhalifu mkubwa wanaofanyiwa na adui Mzayuni mbele ya kimya cha kutisha cha madola ya dunia na mashirika yanayojigamba kutetea haki za binadamu.

Pia amesema, njama za Wazayuni za kuwafarakanisha Wapalestina hazitozaa matunda yanayotakiwa na Wazayuni kwani ukombozi wa ardhi za Palestina umo kwenye damu ya kila Mpalestina.