-
Wazayuni waandamana wakishinikiza kupandishwa kizimbani Benjamin Netanyahu
May 10, 2020 03:12Mamia ya wakazi wa Tel Aviv, mji mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel wamefanya maandamano mjini humo kupinga Baraza la Mawaziri lililoundwa na Benjamin Netanyahu na kushinikiza kupandishwa kizimbari waziri mkuu huyo wa utawala pandikizi wa Kizayuni.
-
Mamluki wa Imarati wawashambulia kwa risasi waandamaji mjini Aden, Yemen
May 10, 2020 03:10Mamluki wa Umoja wa Falme za Kiarabu wamewashambulia kwa risasi watu waliokuwa wanaandamana mjini Aden, kusini mwa Yemen kulalamikia huduma mbovu za umma.
-
Harakati ya Hashdu sh-Sha'abi: Magaidi wa Daesh (ISIS) wamezingirwa jimbo la Diyala
May 09, 2020 23:42Mmoja wa makamanda wa Harakati ya Wananchi ya Hashdu sh-Sha'abi ya nchini Iraq amesema kuwa magaidi wa kundi la Daesh (ISIS) wamezingirwa katika pande nne za jimbo la Diyala, mashariki mwa Iraq.
-
Haniyah: Kuufanya wa kawaida uhusiano na Israel ni kosa lisilosameheka
May 09, 2020 08:03Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema njama zozote zinazolenga kuufanya wa kawaida uhusiano baina ya mataifa ya Kiarabu na utawala haramu wa Israel ni kosa ambalo halina msahama.
-
Netanyahu na jukumu la kuunda serikali ya Israel iliyojaa mikinzano
May 09, 2020 04:40Rais wa utawala wa Kizayuni wa Israel, Reuven Rivlin, amempa jukumu Benjamin Netanyahu la kuunda serikali baada ya kushindwa mara tatu kufikia mwafaka na pande hasimu za kuunda serikali hiyo.
-
Wasiwasi wa Waziri Mkuu wa Pakistan kuhusu harakati za kijeshi za India katika mstari wa udhibiti wa Kashmir
May 09, 2020 03:28Waziri Mkuu wa Pakistan ameonyeshaa wasiwasi mkubwa alionao kuhusiana na harakati mpya za kijeshi za India katika mstari wa udhibiti wa Kashmir (Line of Control) na kuongezeka mashambulio ya jeshi la nchi hiyo dhidi ya mstari huo.
-
Corona yasababisha hasara ya dola bilioni 300 kwa uchumi wa nchi za Kiarabu
May 09, 2020 03:07Mkuu wa umoja wa wawekezaji wa nchi za Kiarabu amesema, uchumi wa nchi hizo umepata hasara ya karibu dola bilioni 323 kutokana na janga la mripuko wa kirusi cha corona.
-
Umoja wa Mataifa wakaribisha na kupongeza kuundwa serikali mpya nchini Iraq
May 08, 2020 06:52Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amekaribisha kwa mikono miwili na kupongeza kuundwa serikali mpya ya Iraq na kusisitiza juu ya kushirikishwa makundi yote katika mchakato wa kisiasa wa nchi hiyo.
-
Ombi la Rais Ashraf Ghani la kutaka Taleban washinikizwe ili wakubali kusitisha vita nchini Afghanistan
May 08, 2020 04:56Katika kikao cha Kundi la Mawasiliano la Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Nchi Zisizofungamana na Siasa za Upande Wowote NAM kilichofanyika kwa njia ya mawasiliano ya intaneti, Rais Muhammad Ashraf Ghani wa Afghanistan ameiomba jumuiya hiyo ilishinikize kundi la Taleban, likubali kusitisha vita nchini humo.
-
HAMAS na Jihadul Islami zapinga mpango wa kufanya mazungumzo na Israel
May 08, 2020 03:45Harakati za Muqawama wa Kiislamu za Palestina HAMAS na Jihadul-Islami zimekosoa vikali mpango wa baadhi ya nchi za Kiarabu wa kutaka kurejea kwenye meza ya mazungumzo na utawala haramu wa Israel.