Wazayuni waandamana wakishinikiza kupandishwa kizimbani Benjamin Netanyahu
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i60887-wazayuni_waandamana_wakishinikiza_kupandishwa_kizimbani_benjamin_netanyahu
Mamia ya wakazi wa Tel Aviv, mji mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel wamefanya maandamano mjini humo kupinga Baraza la Mawaziri lililoundwa na Benjamin Netanyahu na kushinikiza kupandishwa kizimbari waziri mkuu huyo wa utawala pandikizi wa Kizayuni.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
May 10, 2020 03:12 UTC
  • Wazayuni waandamana wakishinikiza kupandishwa kizimbani Benjamin Netanyahu

Mamia ya wakazi wa Tel Aviv, mji mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel wamefanya maandamano mjini humo kupinga Baraza la Mawaziri lililoundwa na Benjamin Netanyahu na kushinikiza kupandishwa kizimbari waziri mkuu huyo wa utawala pandikizi wa Kizayuni.

Kwa mujibu wa shirika la habari la IRNA, jana usiku wakazi wa mji wa Tel Aviv walifanya maandamano hayo kupinga kuruhusiwa Benjamin Netanyahu kuunda serikali licha ya kwamba ana kesi nyingi za ufisadi za kujibu mahakamani. Waandamanaji walitoa maneno makali ya kumlaani Netanyahu kwa ufisadi na ubadhirifu. Siku ya Alkhamisi Bunge la utawala wa Kizayuni (Knesset) lilimruhusu mkuu wa chama cha Likud, Benjamin Netanyahu kuunda serikali kwa kushirikiana na mkuu wa chama cha Buluu na Nyeupe, Benny Gantz. Kwa mujibu wa makubaliano yaliyofikiwa baina ya wawili hao, Benjamin Netanyahu atakuwa Waziri Mkuu wa Israel kwa muda wa mwaka mmoja na nusu, baada ya hapo Benny Gantz atashika wadhifa huo kwa muda kama huo.

Bendera ya utawala wa Kizayuni wa Israel

 

Tangu mwezi Novemba 2018 hadi hivi sasa utawala wa Kizayuni unatikiswa na mkwamo mkubwa wa kisiasa. Mwezi Novemba 2018 Avigdor Lieberman na chama chake cha Yisrael Beiteinu walijitoa kwenye serikali ya Netanyahu hivyo ikalazimika kuitishwa uchaguzi wa kabla ya wakati wake. Uchaguzi huo uliitishwa tarehe 9 Aprili 2019, lakini Netanyahu alishindwa kuunda serikali katika kipindi cha siku 42 alizopewa. Kuna wasiwasi mkubwa kwamba Netanyahu atavunja serikali kabla ya kufikia muda wa kuingia madarakani Gantz. Uhasama na kutoaminiana Wazayuni ni kukubwa kiasi kwamba bunge la Israel limelazimika kutunga sheria ya ajabu ya kumzuia Netanyahu asije akamsaliti Gantz na kuvunja makubaliano waliyofikia. Ijapokuwa kwa hivi sasa mahakama imemuondolea hatia ya ufisadi Netanyahu ili aweze kuunda serikali, lakini wapinzani wake wamesimama imara kuhakikisha anaburuzwa mahakamani kwenda kueleza ni kwa nini amekuwa fisadi.