Pars Today
Rais Faure Gnassingbe wa Togo jana Alkhamisi alimteua tena Victoire Tomegah-Dogbe kuwa waziri mkuu wa nchi hiyo kwa muhula wa miaka sita chini ya katiba mpya.
Vyama vya siasa kali za mrengo wa kulia vimepata mafanikio makubwa katika uchaguzi wa wabunge wa Umoja wa Ulaya, na kutoa kipigo cha kufedhehesha kwa Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Kansela wa Austria Karl Nehammer.
Waziri Mkuu wa Denmark Bi Mette Frederiksen alishambuliwa jana Ijumaa alipokuwa kwenye bustani ya Copenhagen, mji mkuu wa nchi hiyo.
Viktor Orbán, Waziri Mkuu wa Hungary amesema katika taarifa kwamba viongozi wa Umoja wa Ulaya na Jumuiya ya Kujihami ya Kijeshi ya Magharibi (NATO) wanauchukulia mzozo wa Moscow na Kyiv kuwa ni wao na wala hawazingatii hatari ya kujihusisha na mzozo huo. Ameonya kuwa NATO inakaribia kutuma askari wake huko Ukraine.
Ireland ilitangaza Jumatano, Machi 27, kwamba itashiriki katika kesi iliyowasilishwa na Afrika Kusini katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) dhidi ya utawala wa Isarel kutokana na mauaji ya kimbari yanayotekelezwa na utawala huo huko Gaza.
Waziri Mkuu wa Serikali ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina Mohammad Ashtiyah, amejiuzulu wadhifa wake huo.
Pedro Sánchez, Waziri Mkuu wa Uhispania ameonya kuwa, usalama na uthabiti wa eneo la Asia Magharibi (Mashariki ya Kati) umekuwa hatarini na kwamba, mashambulizi haya yanahatarisha nidhamu na uratibu wa ushirikiano wa pande kadhaa.
Waziri Mkuu wa Iraq ameashiria hatua za kuvuruga usalama na amani vya Marekani na kutaka kuondoka nchini humo wanajeshi vamizi wa Marekani haraka iwezekanavyo.
Hatua ya Uhispania na Ubelgiji ya kutangaza kuwa tayari kuitambua rasmi nchi huru ya Palestina ni tukio muhimu kushuhudiwa barani Ulaya kuhusu kadhia ya Palestina. Hatua hii imeukasirisha sana utawala wa Kizayuni.
Waziri Mkuu wa Ireland, Leo Varadkar amekosoa vikali undumilakuwili wa nchi za Magharibi na kusema kuwa Umoja wa Ulaya na madola ya Magharibi yanashughulikia masuala yanayohusiana na Israel na Palestina kwa undumilakuwili wa wazi.