-
Makumi ya watu wafariki dunia katika ajali ya barabarani magharibi mwa Afghanistan
Aug 20, 2025 03:01Msemaji wa Serikali ya Jimbo la Herat magharibi mwa Afghanistan amesema kuwa ajali mbaya ya barabarani katika jimbo hilo imeua watu 71, wakiwemo watoto 17.
-
Kiongozi wa Korea Kaskazini aagiza silaha za nyuklia ziwekwe tayari kukabiliana na Marekani
Aug 19, 2025 23:22Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un, ameitaka nchi yake kuongeza haraka uwezo wake wa nyuklia kutokana na kile alichokitaja kama “uchochezi wazi wa vita” kupitia mazoezi ya kijeshi ya pamoja ya Marekani na Korea Kusini.
-
‘Haikubaliki’: Australia yaikosoa Israel kwa kubatilisha visa za maafisa wake
Aug 19, 2025 23:07Australia imeikosoa Israel kwa kubatilisha visa za mabalozi wake waliokuwa na mamlaka kwa Mamlaka ya Wapalestina, hatua iliyotambuliwa kama ulipizaji kisasi baada ya Canberra kukataa kumkaribisha mwanasiasa wa mrengo wa kulia wa Israel.
-
Mkutano wa Washington kwa ajili ya amani nchini Ukraine; misukumo na changamoto
Aug 19, 2025 22:48Mkutano wa viongozi wa Ulaya na Marekani kuhusu Ukraine ulifanyika mjini Washington siku ya Jumatatu.
-
Ubelgiji kupiga marufuku simu za mkononi maskulini kuanzia mwaka wa masomo wa 2025-2026
Aug 19, 2025 02:42Matumizi ya simu za mkononi na vifaa vingine vya kielektroniki yatapigwa marufuku nchini kote Ubelgiji katika skuli za msingi na sekondari kuanzia mwaka wa masomo wa 2025-2026, isipokuwa vitakapolazimu kutumika kwa sababu za kimasomo, kiafya, au za dharura. Hayo yameripotiwa na vyombo vya habari vya ndani ya nchi hiyo.
-
Israel yazuiwa kushiriki maonyesho ya biashara ya Italia
Aug 18, 2025 23:36Utawala wa kizayuni wa Israel umepigwa marufuku kushiriki katika maonyesho ya biashaya Italia.
-
Waliokufa kwa maafa ya mafuriko Pakistan wapindukia 600
Aug 18, 2025 23:23Idadi ya watu waliopoteza maisha kufuatia janga la mafuriko nchini Pakistan imeongezeka na kupindukia 600.
-
Kwa nini viongozi wa Ulaya wanaandamana na Zelensky katika safari yake ya Washington?
Aug 18, 2025 23:15Baadhi ya viongozi wa Ulaya, wameamua kuandamana na Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine katika safari yake ya kwenda Washington katika hatua ya kidiplomasia ya kuunga mkono misimamo ya Ukraine katika mazungumzo yake na Rais Donald Trump wa Marekani dhidi ya mashinikizo ya nchi hiyo ya kumtaka akubali haraka makubaliano ya amani.
-
Makanisa ya Uholanzi yatangaza kuitambua Palestina
Aug 18, 2025 07:26Makanisa 73 ya Kiprotestanti nchini Uholanzi yametoa taarifa ya kuitaka serikali ya nchi hiyo kulitambua taifa la Palestina na kuacha kupeleka shehena ya silaha kwa utawala wa kizayuni wa Israel.
-
Uruguay yafunga ofisi yake Quds kuonyesha mshikamano na Gaza
Aug 17, 2025 23:24Serikali ya Uruguay imeamua kusitisha makubaliano ya ushirikiano yaliyotiwa saini mwezi Disemba mwaka jana 2024 kati ya Wakala wa Kitaifa wa Utafiti na Ubunifu wa Uruguay na chuo kikuu cha Israel huko Quds (Jerusalem) inayokaliwa kwa mabavu, sanjari na kufunga Ofisi yake ya Ubunifu mjini Jerusalem ili kuonyesha mshikamano na Wapalestina wa Ukanda wa Gaza.