-
Macron akiri ukandamizaji wa Ufaransa katika makoloni yake
Aug 13, 2025 08:18Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amekiri makosa ya nchi yake katika makoloni yake kabla, wakati na baada ya uhuru wa mataifa hayo ikiwemo Cameroon na Senegal.
-
Brazil yatoa wito wa kusitishwa vita mara moja katika Ukanda wa Gaza
Aug 13, 2025 07:29Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva amesisitizia ulazima wa kufikiwa mara moja usitishaji vita kamili katika Ukanda wa Gaza na kuondolewa kikamilifu kwa vikosi vya Israel vinavyokalia kwa mabavu katika eneo hilo.
-
Amnesty International yataka kukomeshwa mauaji huko Gaza
Aug 12, 2025 23:01Shirika la Msamaha Duniani la Amnesty International limetoa wito wa kuchukuliwa hatua za haraka za kimataifa kukomesha mauaji katika Ukanda Gaza.
-
Norway: Tuko tayari kutekeleza agizo la ICC la kukamatwa Netanyahu
Aug 12, 2025 23:00Naibu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Norway ametangaza kuwa, iwapo Benjamin Netanyahu Waziri Mkiuu wa Israel ataizuru nchi hiyo, Oslo itatekeleza agizo la kukamatwa lililotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC).
-
Utunishaji misuli wa Trump katika mji mkuu wa Marekani; kuongezeka maandamano dhidi ya Gadi ya Ulinzi wa Taifa
Aug 12, 2025 22:59Rais Donald Trump wa Marekani, amesema kwamba ataongeza uwepo wa vikosi vya polisi vya shirikisho katika mji mkuu wa nchi hiyo, kwa kisingizio cha kuongezeka vitendo vya uhalifu huko Washington DC.
-
Umoja wa Ulaya walaani mauaji ya waandishi wa habari wa Al Jazeera yaliyofanywa na utawala wa Kizayuni
Aug 12, 2025 09:55Umoja wa Ulaya umelaani mauaji ya waandishi wa habari wa Televisheni ya Al Jazeera na utawala wa Kizayuni na kusisitiza kwamba waandishi wa habari hawapaswi kulengwa.
-
Norway yasimamisha uwekezaji katika makampuni 11 ya Israel
Aug 12, 2025 09:42Hazina ya Utajiri wa Taifa wa Norway imetangaza kuwa imesitisha uwekezaji katika makampuni 11 ya utawala wa Israel ambayo yamewekeza katika kampuni ya utengenezaji wa injini za ndege.
-
Mbunge mwandamizi wa UK asema ni dhahiri kwamba balozi wa Marekani Israel ni 'mpumbavu'
Aug 12, 2025 03:51Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje ya bunge la Uingereza Emily Thornberry amesema, ni dhahiri kuwa balozi wa Marekani katika utawala wa kizayuni wa Israel Mike Huckabee ni 'mpumbavu' kufuatia matamshi yake ya kuikosoa Uingereza kwa kupinga mpango wa Israel wa kuuvamia na kuukalia kwa mabavu kikamilifu Ukanda wa Ghaza.
-
Rais wa Uturuki: Baada ya miaka 80 lazima UN ifanyiwe mageuzi makubwa ili kutimiza wajibu wake
Aug 12, 2025 03:28Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki amesema, wakati Umoja wa Mataifa unakaribia kuadhimisha miaka 80 ya kuasisiwa kwake ni wazi kwamba unahitaji mabadiliko makubwa ili kuendelea kutekeleza majukumu uliyopewa.
-
Takwa jipya la Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa Jamii ya Kimataifa kuhusu utawala wa Kizayuni
Aug 12, 2025 02:35Francesca Albanese, Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa ametoa wito wa kufukuzwa timu za michezo za utawala wa Kizayuni katika mashindano ya kimataifa.