Norway: Tuko tayari kutekeleza agizo la ICC la kukamatwa Netanyahu
https://parstoday.ir/sw/news/world-i129464
Naibu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Norway ametangaza kuwa, iwapo Benjamin Netanyahu Waziri Mkiuu wa Israel ataizuru nchi hiyo, Oslo itatekeleza agizo la kukamatwa lililotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC).
(last modified 2025-08-13T02:30:20+00:00 )
Aug 13, 2025 02:30 UTC
  • Norway: Tuko tayari kutekeleza agizo la ICC la kukamatwa Netanyahu

Naibu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Norway ametangaza kuwa, iwapo Benjamin Netanyahu Waziri Mkiuu wa Israel ataizuru nchi hiyo, Oslo itatekeleza agizo la kukamatwa lililotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC).

Andreas Kravik  amesema kuwa, hatua za utawala wa kizayuni hazikubaliki kabisa. Tumeshuhudia mashambulizi dhidi ya shule, hospitali na waandishi wa habari.

Serikali ya Norway kupitia naibu waziri wake huyo imesema, kutokana na hali hiyo, serikali ya nchi hiyo itamtia mbaroni Benjamin Netanyahu endapo ataingia nchini humo.

Msimamo wa Norway unaweza kusababisha wimbi la hatua kama hizo huko barani Ulaya hasa katika kipindi hiki ambapo kuna kampeni kubwa dhidi ya Israel kutokana na jinai zake dhidi ya wakazi wa Uukanda wa Gaza. Iwapo nchi nyingi zitajitolea kutekeleza uamuzi wa mahakama ya ICC, Netanyahu atakabiliwa na vikwazo vikali vya usafiri wa nje. Inaweza pia kuathiri uchunguzi wa kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita huko Gaza.

Novemba mwaka jana (2024), Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC ilitoa hati za kukamatwa waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na Yoag Gallant aliyekuwa waziri wake wa vitaa baada ya kuwafungulia mashtaka ya kutenda jinai za kivita na jinai dhidi ya binadamu huko Gaza, ambako utawala wa Kizayuni umekuwa ukiendesha vita vya kinyama na kufanya mauaji ya kimbarii tangu mwezi wa Oktoba mwaka jana.