Uingiliaji wa Marekani na Uingereza wawakasirisha wananchi wa Iraq
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i129472
Uingiliaji wa Marekani na Uingereza katika masuala ya ndani ya Iraq umeibua hasira miongoni mwa wabunge wa nchi hiyo ya Asia Magharibi.
(last modified 2025-08-13T05:12:21+00:00 )
Aug 13, 2025 05:12 UTC
  • Uingiliaji wa Marekani na Uingereza wawakasirisha wananchi wa Iraq

Uingiliaji wa Marekani na Uingereza katika masuala ya ndani ya Iraq umeibua hasira miongoni mwa wabunge wa nchi hiyo ya Asia Magharibi.

 

Rafiq al-Swalihi, mwanachama wa mrengo wa aS-Swadiqoun katika Bunge la Iraq, ameikosoa vikali Marekani kwa kutumia ushawishi wake katika sekta ya mafuta ya Iraq kama kichocheo cha kutoa mashinikizo ya kiuchumi na kisiasa dhidi ya serikali ya Baghdad.

Naye Ala Al-Haydari, mjumbe wa bunge la Iraq, amekosoa vikali uingiliaji  wa balozi wa Uingereza nchini Iraq na kuhoji: Ni nani aliyempa balozi wa Uingereza haki ya kusimamia masuala ya Iraq?

Yassir al-Husseini, mbunge mwingine wa Bunge la Iraq naye amekosoa vikali uingiliaji wa balozi wa Marekani na Uingereza katika masuala ya ndani ya Iraq na kusema: Al-Hashd al-Shaabi ni taasisi ya kitaifa ambayo ilianzishwa kwa fatwa yenye mamlaka ya kidini na ni halali. Hivyo hakuna upande wowote utakaoruhusiwa kuingilia kati. Balozi wa Uingereza nchini Iraq ni mtu asiyetakikana tena kuwepo nchini na amechukua hatua iliyo kinyume na shughuli za kidiplomasia kufuatia matamshi yake ya hivi karibuni.