WHO yataka misaada zaidi kuingia katika Ukanda wa Gaza
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i129484-who_yataka_misaada_zaidi_kuingia_katika_ukanda_wa_gaza
Shirika la Afya Duniani (WHO), limeutaka utawala wa kizayuni wa Israel uliruhusu kupeleka vifaa ya matibabu katika Ukanda wa Gaza ili kushughulikia janga la kiafya huko kabla ya Israel haijachukua udhibiti kamili wa ukanda huo.
(last modified 2025-11-16T06:33:27+00:00 )
Aug 13, 2025 11:00 UTC
  • Wato wa Gaza wakisubiria chakula cha msaada.
    Wato wa Gaza wakisubiria chakula cha msaada.

Shirika la Afya Duniani (WHO), limeutaka utawala wa kizayuni wa Israel uliruhusu kupeleka vifaa ya matibabu katika Ukanda wa Gaza ili kushughulikia janga la kiafya huko kabla ya Israel haijachukua udhibiti kamili wa ukanda huo.

Rik Peeperkorn, mwakilishi wa shirika hilo kwenye maeneo ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu amesema kuwa, wanataka kupeleka vifaa hivyo Gaza. Afisa huyo wa WHO ameeleza kuwa misaada ya kibinaadamu haifikishwi ipasavyo katika ukanda huo licha ya taarifa za awali kusema misaada inafikishwa katika Ukanda huo unaokumbwa na vita.

"Tunataka kuhakikisha kwamba, angalau hospitali zinakuwa na vifaa vya kutosha pamoja na dawa. Kwa sasa hatuwezi kufanya hivyo, tunataka pia kujaza upya hifadhi zetu lakini hatuwezi kwa sasa kufanya hivyo kwa njia inayofaa. Taratibu ni lazima ziwekwe. Tunahitaji kupeleka dawa zote na vifaa vinavyohitajika. Na simaanishi kwa ajili ya afya pekee, lakini pia chakula, masoko lazima yajazwe vyakula, maji, mafuta na kadhalika," alisema Peeperkorn.

Rik Peeperkorn, mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kwenye maeneo ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu

 

Mashirika ya Umoja ya Mataifa yalionya mwezi uliopita kwamba baa la njaa linashuhudiwa Gaza, huku Israel ikizuwia misaada kufikishwa huko. Takriban watoto 12,000 walio chini ya miaka mitano walitambuliwa kuugua utapiamlo mwezi Julai ikiwa ni idadi ya juu kuwahi kurekodiwa Gaza.

Timu ya wataalamu wa Umoja wa Mataifa imelaani hatua ya Israel ya kuzidisha kampeni yake ya mauaji ya kimbari dhidi ya watu wa Palestina huko Gaza na kuitaka jamii ya kimataifa kukomesha "ushiriki" wake katika uhalifu wa Israel na kukabiliana na ukatili wa utawala huo.