Uingereza yakabiliwa na umasikini ambao haujawahi kushuhudiwa
https://parstoday.ir/sw/news/world-i129514
Uingereza inakabiliwa na umaskini mbaya zaidi katika kipindi cha miaka 60 iliyopita, huku idadi ya kaya zisizo na mahitaji ya msingi ikiongezeka sana.
(last modified 2025-08-14T09:10:40+00:00 )
Aug 14, 2025 06:41 UTC
  • Uingereza inakabiliwa na umaskini mbaya zaidi katika kipindi cha miaka 60 iliyopita.
    Uingereza inakabiliwa na umaskini mbaya zaidi katika kipindi cha miaka 60 iliyopita.

Uingereza inakabiliwa na umaskini mbaya zaidi katika kipindi cha miaka 60 iliyopita, huku idadi ya kaya zisizo na mahitaji ya msingi ikiongezeka sana.

Hali hii ni dalili ya mgogoro mkubwa zaidi wa kijamii ambao unaweza kuwa na madhara makubwa kwa afya ya akili na ubora wa maisha ya mamilioni ya watu nchini Uingereza. Kuongezeka kwa umaskini, hasa miongoni mwa watoto, kumezua wasiwasi mkubwa kuhusu mustakabali wa kijamii na kiuchumi wa nchi hiyo ya Ulaya.

Gazeti la The Independent limeandika katika moja ya makala zake: Kaya za Uingereza ambazo hazina angalau mahitaji mawili kati ya saba ya msingi, kama vile chakula, vifaa vya usafi au nyumba, sasa zinaongezeka, na aina hii ya umaskini inaenea kwa kasi zaidi kuliko umaskini mkubwa katika nchi hiyo ya

Pia, 56% ya maskini nchini Uingereza wanaishi katika familia zinazofanya kazi na idadi ya kaya ambazo zimekumbwa na umaskini mkubwa imeongezeka kwa kasi. Ikilinganishwa na miaka ya 1970, idadi ya watoto walio katika umaskini nchini Uingereza imeongezeka maradufu, huku watoto milioni 4.5 sasa wakikulia katika mazingira ya umaskini nchini Uingereza.

Katika miongo ya hivi karibuni, utekelezaji wa sera za kubana matumizi, upunguzaji wa misaada kwa wahitaji, vita, kupanda kwa mfumuko wa bei, na gharama ya maisha kumeongeza kiwango cha umaskini katika jamii za Uingereza.