-
Uswahiba wa Trump na Elon Musk wazidi kuharibika baada ya kurushiana matusi
Jun 06, 2025 22:59Uswahiba huba wa Rais wa Marekani Donald Trump na mfanyabiashara tajiri zaidi duniani Elon Musk sasa unaonekana kufikia ukingoni baada ya wawili hao kurushiana cheche za maneno makali na hata matusi kwenye mitandao ya kijamii.
-
Je, licha ya maonyo haya yote, wanaodao kutetea haki za binadamu wako wapi?
Jun 06, 2025 22:40Zaidi ya watu milioni 2 katika Ukanda wa Gaza wanakabiliwa na baa la njaa kali, huku jamii ya kimataifa ikiamua kukaa kimya tu na kutochukua hatua yoyote ya maana ya kuokoa maisha ya watu hao wanaoendelea kuteseka chini ya ukandamizaji na jinai za kutisha za utawala wa Kizayuni kwa ushirkiano wa serikali za Marekani na nchi nyingine za Magharibi.
-
Mamilioni ya Waislamu nchini Iran na duniani kote waadhimisha Sikukuu ya Idul Adh'ha
Jun 06, 2025 08:12Mamilioni ya Waislamu nchini Iran na sehemu mbalimbali za dunia leo wameaadhimisha Sikukuu ya Idul Adh'ha , moja ya sikukuu muhimu zaidi katika kalenda ya Kiislamu ,kwa sala, sadaka, na desturi ya kuchinja kwa ajili ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu.
-
Trump: Biden alitia saini maelfu ya hati bila ya kujielewa
Jun 06, 2025 03:17Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kuwa ameanzisha uchunguzi kuhusu utendaji kazi wa Joe Biden akidai kuwa maelfu ya hati na maagizo ya kiutendaji yalitolewa kwa kutumia saini zilizoandikwa na mashine na bila umma kujua.
-
Pentagon yaanza uchunguzi kuhusu kufeli Marekani Yemen
Jun 05, 2025 23:00Duru za kijeshi za Marekani zimeliambia jarida la Wall Street Journal kwamba wizara ya ulinzi ya nchi hiyo Pentagon imeanzisha uchunguzi wa kina kuhusu sababu za kushindwa Marekani katika vita vyake na Wahouthi na kudai kuwa kushindwa huko kunashangaza.
-
Waandishi Wahispania wataka kuhitimishwa vita Gaza
Jun 05, 2025 22:59Waandishi zaidi ya 400 wa Uhispania wamesema kuwa, utawala wa Israel umekiuka sheria za kimataifa na wametoa mwito wa kusitishwa mara moja mashambulizi ya utawala huo dhidi ya Gaza.
-
Kuanzia Italia hadi Japan, watu wote wanaichukia Israel
Jun 05, 2025 09:30Mitazamo hasira na ya ghadhabu dhidi ya Israel inaendelea kuongezeka duniani kutokana na jinai za utawala wa Kizayuni huko Ghaza. Chuki na hasira hizo dhidi ya Israel zinaongezeka hata katika nchi ambazo kwa jadi zinauunga mkono kwa nguvu utawala wa Kizayuni, kama vile Hungary na Poland.
-
Kwa nini Trump ameshindwa kutatua migogoro ya kimataifa licha ya ahadi zote alizotoa?
Jun 05, 2025 02:28Katika makala yake iliyopitia miezi minne ya kwanza ya utawala wa pili wa Donald Trump, tovuti ya CNN imeandika kwamba kabla ya kuingia madarakani, rais huyo alijigamba kwamba alikuwa na uwezo wa kutatua matatizo na migogoro mikubwa ya dunia, lakini hali ya sasa sio nzuri hata kidogo, ingawa yeye si rais pekee wa Marekani kutoa ahadi za uongo kuhusu suala hilo.
-
Akthari ya Waingereza wanataka Israel iwekewe vikwazo
Jun 04, 2025 23:40Utafiti mpya wa maoni uliosimamiwa na Kampeni ya Mshikamano na Palestina (PSC) unaonyesha kuwa, aghalabu ya wananchi wa Uingereza wanaunga mkono kuwekwa vikwazo kamili vya kijeshi dhidi ya utawala wa Israel.
-
Kwa nini nchi za Amerika ya Latini zimejiunga na safu ya wakosoaji wa Israel?
Jun 03, 2025 22:57Rais Lula da Silva wa Brazil amesisitiza katika matamshi yake kwamba kinachoendelea Gaza si vita bali ni mauaji ya halaiki. Alifafanua: Tunachoshuhudia huko Gaza hivi sasa si vita kati ya majeshi mawili hata kidogo, bali kuna jeshi moja tu lenye weledi kamili ambalo linaua wanawake na watoto wa Ukanda wa Gaza.