-
Trump apinga marekebisho ya sheria ya haki ya kubeba silaha
Apr 19, 2025 02:31Rais Donald Trump wa Marekani ametangaza kuwa hana mpango wa kufanyia marekebisho sheria ya haki ya kubeba silaha nchini humo licha ya kushuhudia mara kwa mara ufyatuaji risasi mashuleni na katika vituo vya elimu nchini humo.
-
Wasiwasi wa Ulaya uliotokana na mgeuko mkubwa katika sera za Marekani kuhusiana na washirika wake
Apr 18, 2025 22:55Kubadilika sera za nje za Marekani kumeanza kidogo kidogo kuwatoa mafichoni wanasiasa wa Ulaya kwa kuwafanya waeleze kinagaubaga na kwa uwazi zaidi wasiwasi walionao kuhusu sera za Donald Trump za kujichukulia hatua za upande mmoja.
-
Wayahudi wa Uingereza walaani vita vya Israel dhidi ya watu wa Gaza
Apr 18, 2025 22:53Wawakilishi kadhaa wa jamiii ya Wayahudi nchini Uingereza wamelaani sera za serikali ya Benjamin Netanyahu, wakiishutumu kwa kutenda kinyume na "maadili ya Kiyahudi" kuhusiana na vita dhidi ya watu wa Gaza huko Palestina.
-
UN yapinga kuondolewa Taliban kwenye orodha iliyopigwa marufuku ya Russia
Apr 18, 2025 22:51Kufuatia uamuzi wa Mahakama ya Juu ya Russia wa kuliondoa kundi la Taliban kwenye orodha ya mashirika yaliyopigwa marufuku, Umoja wa Mataifa umetangaza kwamba hatua hiyo haibadilishi hadhi ya Taliban katika taasisi hiyo na kwamba vikwazo vya kimataifa dhidi ya kundi hilo vitaendelea kuwepo.
-
Trump kufunga balozi 30 za Marekani duniani, zaidi ya nusu ziko Afrika
Apr 18, 2025 10:11Utawala wa Trump unapanga kupunguza makumi ya balozi za Marekani duniani kote, ambapo umependekeza kufunga balozi na balozi ndogo karibu 30, zaidi ya nusu zikiwa barani Afrika.
-
Kushadidi mashinikizo na ukandamizaji wa Magharibi dhidi ya watetezi na waungaji mkono wa Palestina
Apr 18, 2025 04:05Sambamba na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel kuendeleza vita vya kinyama na mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina wa Ghaza na kuzuia kikamilifu misaada ya kibinadamu isiingizwe katika eneo hilo uliloliwekea mzingiro, nchi za Magharibi zinazouunga mkono utawala huo ghasibu hususan Ujerumani na Marekani nazo pia zimeshadidisha mashinikizo na ukandamizaji dhidi ya watetezi na waungaji mkono wa Palestina.
-
ICJ yaafikiana na Israel kuakhirisha kesi ya mauaji ya halaiki Gaza kwa miezi 6
Apr 18, 2025 03:15Katika hatua inayotia wasiwasi, Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) imeafiki ombi la kuakhirisha kesi iliyowasilishwa na Afrika Kusini dhidi ya Israel, kuhusu kampeni ya kikatili na ya kijeshi ya utawala huo wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza.
-
ICC yaifungulia mashtaka Hungary kwa kutomkamata Netanyahu
Apr 17, 2025 23:04Mahakama ya Kimataifa ya Jinai imefungua rasmi kesi dhidi ya Hungary baada ya serikali ya Budapest kukataa kutekeleza waranti wa ICC wa kumkamata waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu wakati wa ziara yake rasmi nchini humo mapema mwezi huu.
-
NYT: Trump alipinga pendekezo la Israel la kushambulia vituo vya nyuklia vya Iran
Apr 17, 2025 09:11Rais wa Marekani, Donald Trump amekataa pendekezo la Israel la kushambulia vituo vya nyuklia vya Iran, gazeti la New York Times liliripoti hayo Jumatano jioni, likiwanukuu maafisa wa Ikulu ya White House na maafisa wengine wanaofahamu suala hilo.
-
Wafungwa Waislamu ‘wanalengwa’ na kukandamizwa nchini UK
Apr 16, 2025 23:00Shirika moja la kupigania haki za kijamii limefichua kwamba, wafungwa Waislamu nchini Uingereza wananyanyaswa na kuwekewa mbinyo, ikiwa ni pamoja na kupigwa marungu na kuwekewa vizuizi hasa katika magereza yenye Waislamu wengi.