-
CNN: Marekani imejitenga na nchi za Magharibi katika suala la Ukraine
Feb 26, 2025 03:07Televisheni ya CNN ya Marekani imetangaza kuwa: Washington imejitenga na nchi za Magharibi kuhusu suala la Ukraine, na hili ndilo jambo lililobadilishwa na Donald Trump kuhusu nafasi ya Marekani kimataifa.
-
Jumuiya ya ASEAN na udharura wa kusaidia kutatua mgogoro wa Waislamu wa Rohingya
Feb 25, 2025 22:47Sambamba na mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Mashhauri ya Kigeni wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Mataifa ya Kusini Mashariki mwa Asia (ASEAN) huko Langkawi, Malaysia, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa nchi hiyo amesisitiza dhamira ya Kuala Lumpur kama mwenyekiti wa zamu wa umoja huo juu ya kutatuliwa mgogoro wa Myanmar na kurejesha amani ya nchi hiyo.
-
EU: Hatuwezi kuficha wasiwasi tulionao kuhusu matukio yanayojiri Ufukwe wa Magharibi, Palestina
Feb 25, 2025 06:15Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya amesema, umoja huo hauwezi kuficha wasiwasi ulionao kuhusu matukio yanayojiri katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kwamba mzozo wa Palestina na Israel hauna ufumbuzi mwingine isipokuwa suluhu ya kuundwa mataifa mawili.
-
The Economist: Ukraine inahitaji muda wa karne kadhaa kuweza kulipa deni la fedha kwa Marekani
Feb 25, 2025 06:15Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na gazeti la The Economist linalochapishwa nchini Uingereza, ikiwa Ukraine itatia saini makubaliano na Marekani ya kulipa fidia ya dola bilioni 500, kwa kuzingatia kasi yake ya sasa ya ukuaji wa uchumi, itahitaji mamia ya miaka ili kuweza kulipa deni lake hilo.
-
"Ulaya ndiyo iliyopata hasara kubwa katika kamari ya Trump na Putin"
Feb 25, 2025 02:29Wakati huu ambapo Saudi Arabia inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mkutano baina ya marais wa Russia na Marekani, kila kitu kinathibitisha kwamba aliyepata hasara kubwa katika kamari hiyo ni nchi za Ulaya.
-
Shirika la DAWN lataka ICC imchunguze Rais wa Marekani
Feb 24, 2025 23:27Shirika moja lisilo la serikali limeitaka Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) kuanzisha uchunguzi dhidi ya Rais Donald Trump wa Marekani, kutokana na mienendo yake dhidi ya maafisa wa korti hiyo ya kimataifa iliyoko The Hague huko Uholanzi.
-
Hungary: Baadhi ya nchi za Ulaya zinakwamisha kumalizika vita huko Ukraine
Feb 24, 2025 22:54Waziri wa Mambo ya Nje wa Hungary amesema kuwa "Waliberali wa Ulaya wanaounga mkono vita" wanakwamisha kufanyika mazungumzo ya amani kati ya Marekani na Russia ili kuhitimisha vita huko Ukraine.
-
Afisa wa polisi wa Kenya auawa Haiti akilinda doria
Feb 24, 2025 08:54Afisa wa polisi wa Kenya aliyepelekwa Haiti chini ya mpango wa Kikosi cha Kimataifa cha Kulinda Usalama Haiti (MSS) amefariki dunia baada ya kupigwa risasi akiwa kwenye doria.
-
Vatican: Hali ya kiafya ya Papa Francis ni mbaya kutokana na tatizo la kupumua
Feb 23, 2025 07:36Vatican imetangaza kuwa hali ya kiafya ya kiongozi wa Kanisa Katoliki mwenye umri wa miaka 88 bado ni mbaya.
-
WHO yasisitiza kuhusu makubaliano ya kuzuia majanga
Feb 22, 2025 23:11Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Tedros Adhanom Ghebreyesus, ameonya kuwa historia haitazisamehe nchi ikiwa zitashindwa kuingia katika makubaliano ya kuzuia kwa pamoja majanga ya siku zijazo.