CNN: Marekani imejitenga na nchi za Magharibi katika suala la Ukraine
https://parstoday.ir/sw/news/world-i123220-cnn_marekani_imejitenga_na_nchi_za_magharibi_katika_suala_la_ukraine
Televisheni ya CNN ya Marekani imetangaza kuwa: Washington imejitenga na nchi za Magharibi kuhusu suala la Ukraine, na hili ndilo jambo lililobadilishwa na Donald Trump kuhusu nafasi ya Marekani kimataifa.
(last modified 2025-02-26T06:37:24+00:00 )
Feb 26, 2025 06:37 UTC
  • CNN: Marekani imejitenga na nchi za Magharibi katika suala la Ukraine

Televisheni ya CNN ya Marekani imetangaza kuwa: Washington imejitenga na nchi za Magharibi kuhusu suala la Ukraine, na hili ndilo jambo lililobadilishwa na Donald Trump kuhusu nafasi ya Marekani kimataifa.

CNN imeripoti kuwa Marekani imeonyesha kusitasita kulaani uchokozi wa Kremlin katika kumbukumbu ya mwaka wa tatu wa uvamizi wa kikatili nchini Ukraine siku ya Jumatatu iliyopita, kwa kuchagua marafiki wapya katika Umoja wa Mataifa, wakiwemo mahasimu wake wa muda mrefu, yaani Russia na Korea Kaskazini.

Ripoti ya CNN imesema, matukio ambayo hayajawahi kushuhudiwa hapo kabla katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa yalikuwa bora zaidi kuliko yale ya Ikulu ya White House, ambapo Trump na mwenzake wa Ufaransa, Emmanuel Macron, walipeana mikono na kufanyiana unafiki, na hivyo kuonyesha mgawanyiko mpya kati ya pande mbili za Bahari ya Atlantiki.

Ripoti ya CNN imeongeza kuwa, mwelekeo wa kutatanisha wa Trump kwa Putin na kujitenga na Ukraine umevuruga miungano ya zamani na kuanzisha ushindani wa washirika na wapinzani wa Marekani kwa ajili ya kuunda makubaliano ya amani ambayo anakusudia kufanya na kiongozi wa Urusi.