Idadi ya mashahidi huko Gaza imefikia 68,527
Oct 28, 2025 05:51 UTC
-
Idadi ya mashahidi huko Gaza imefikia 68,527
Wizara ya Afya ya Palestina imetangaza kuwa, idadi ya Wapalestina waliouawa shahidi katika mashambulizi ya jeshi la Israel Ukanda wa Gaza imefikia 68,527.
Taasisi hiyo ya matibabu ya Palestina pia imeeleza kuwa, jumla ya watu waliojeruhiwa katika mashambulizi ya jeshi la Israel kwenye Ukanda wa Gaza tangu kuanza kwa vita katika Ukanda huo Oktoba mwaka 2023 imefikia 170,395.
Wizara hiyo imetangaza kuwa katika muda wa saa 48 zilizopita, miili ya mashahidi 8 pia imehamishiwa hospitalini, 8 kati yao ikiwa imetolewa kutoka chini ya vifusi. Watu 13 pia wamejeruhiwa katika kipindi hiki. Maelfu ya wengine bado hawajulikani walipo kutokana na kufukiwa chini ya vifusi katika Ukanda wa Gaza.