CPJ: Waandishi wa Habari wa Kipalestina wanateswa katika magereza ya Israel
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i136810-cpj_waandishi_wa_habari_wa_kipalestina_wanateswa_katika_magereza_ya_israel
Kamati ya Kimataifa ya Kuwalinda Waandishi wa Habari (CPJ) imetangaza kuwa,  waandishi habari wa Kipalestina waliofungwa katika magereza ya utawala ghasibu wa Israel kuanzia Oktoba 2023 hadi Januari 2026 wamepitia "unyanyasaji wa kimfumo."
(last modified 2026-02-19T12:09:32+00:00 )
Feb 19, 2026 12:09 UTC
  • CPJ: Waandishi wa Habari wa Kipalestina wanateswa katika magereza ya Israel
    CPJ: Waandishi wa Habari wa Kipalestina wanateswa katika magereza ya Israel

Kamati ya Kimataifa ya Kuwalinda Waandishi wa Habari (CPJ) imetangaza kuwa,  waandishi habari wa Kipalestina waliofungwa katika magereza ya utawala ghasibu wa Israel kuanzia Oktoba 2023 hadi Januari 2026 wamepitia "unyanyasaji wa kimfumo."

Taarifa ya shirika hilo lenye makao yake makuu jijini New York Marekani  imesema, kati ya waandishi 59 waliohojiwa, wote isipokuwa mmoja walisema walifanyiwa kile walichoelezea kuwa ni  wa haki za binadamu. Mkurugenzi wa CPJ Jodie Ginsberg ameihimiza jamii ya kimataifa "kuchukua hatua" kuhusu ripoti hizo za unyanyasaji.

Taarifa ya CPJ imesema, jeshi la utawala vamizi wa Israel halikutoa kauli kuhusu madai hayo yaliyotolewa. Hata hivyo, msemaji mmoja alisema wafungwa "hushughulikiwa kwa mujibu wa sheria za kimataifa."

Hivi karibuni Shirika la Waandishi wa Habari Bila Mipaka (RSF) lilitangaza kuwa, utawala wa Israel ni muuaji mkuu wa waandishi wa habari duniani kwa mwaka wa tatu mfululizo, na likautaka utawala huo uwajibike kwa kusababisha karibu nusu ya vifo vya waandishi wa habari duniani mwaka 2025, hasa katika Ukanda wa Gaza unaozingirwa.

Israel imekuwa ikiwaita waandishi wa habari wengi wa Kipalestina kama magaidi, huku RSF ikiripoti kwamba utawala wa Israel umeanzisha kampeni ya kumchafua waandishi wa habari wa Gaza, ikiwa ni pamoja na kuwapa lebo za kifo.

Waandishi wa habari wa kigeni bado wanazuizi kubwa kuingia katika eneo lililoathirika na vita la Gaza, wakiwa wamezuiliwa katika ziara zinazodhibitiwa na jeshi la Israel, licha ya wito wa mara kwa mara kutoka kwa vikundi vya uhuru wa vyombo vya habari kwa ufikiaji huru.