-
Katibu Mkuu wa UN aionya Israel: Kushambulia askari wa UNIFIL inaweza ikawa jinai ya kivita
Oct 14, 2024 03:58Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameutahadharisha utawala wa Kizayuni wa Israel kwamba, kuwashambulia walinda amani wa umoja huo kunakiuka sheria za kimataifa, ikiwa ni pamoja na sheria za kimataifa za kibinadamu na kwamba ukiukaji huo unaweza kuwa uhalifu wa kivita.
-
Mshindi wa Nobel: Hali ya watoto wa Ghaza ni kama ya wa Japan baada ya Vita vya Pili vya Dunia
Oct 14, 2024 02:08Kundi la Nihon Hidankyo, mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel ya 2024 limesema, hali ya watoto katika Ukanda wa Ghaza ni sawa na hali ya watoto wa Japan ilivyokuwa mwishoni mwa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.
-
Kikao cha Moscow na suala la wahamiaji wa Afghanistan
Oct 13, 2024 22:54Mjumbe Maalumu wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika masuala ya Afghanistan amesema kuwa kikao kilichofanywa hivi karibuni na nchi jirani za Afghanistan huko Moscow, kilifanyika katika fremu ya mpango wa kikanda wa kuisaidia Afghanistan katika kupambana na ugaidi na kuisaidia kupata maendeleo, ili kuepusha wimbi la wahamiaji kutoka nchi hiyo.
-
Indonesia yayatolea wito mataifa ya Asia Mashariki kuitambua nchi ya Palestina
Oct 13, 2024 06:02Indonesia imetoa wito kwa mataifa ya Asia Mashariki kuitambua nchi ya Palestina na kuitaka jamii ya kimataifa isimamie sheria za kimataifa na ubinadamu.
-
Ishiba: Sitasahau kamwe mshtuko niliopata kwa taswira ya bomu la nyuklia la US Hiroshima
Oct 13, 2024 05:36Waziri Mkuu wa Japan Shigeru Ishiba amesema, anataka "ghaya na lengo kuu" liwe ni la kuwa na dunia isiyo na silaha za nyuklia huku akikumbusha kile alichokiita tajiriba ya kushtusha aliyopata alipoona video inayoonyesha Marekani ikishambulia mji wa Hiroshima nchini Japan kwa bomu la nyuklia na kusisitiza kwamba anataka kuhakikisha majanga ya aina hiyo hayawezi kutokea tena.
-
Mtikisiko wa kiuchumi US; Boeing kuwatimua wafanyakazi 17,000
Oct 12, 2024 22:44Kampuni ya Boeing inayoongoza nchini Marekani kutengeneza ndege za kibiashara na kijeshi imetangaza mpango wake wa kuwapiga kalamu nyekundu wafanyakazi 17,000 wa shirika hilo; huku mgomo wa wafanyakazi 33,000 wa kampuni hiyo huko West Coast ukitokota.
-
Kuundika mwafaka wa kimataifa dhidi ya Israel
Oct 12, 2024 22:39Utawala wa Kizayuni unaendelea kulaaniwa na kukosolewa pakubwa kimataifa kufuatia kuendelea jinai kubwa za utawala huo katika vita vya Gaza hususan mauaji ya kimbari unayotekekeleza dhidi ya Wapalestina na hivi sasa mashambulizi ya kila upande dhidi ya Lebanon ambayo yamewaua shahidi maelfu ya watu na kujeruhi makumi ya maelfu ya wengine huko Gaza na Lebanon.
-
Umoja wa Mataifa: Israel imefanya uhalifu wa kivita katika Ukanda wa Gaza
Oct 12, 2024 03:51Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel umetekeleza uhalifu wa kivita katika Ukanda wa Gaza.
-
Nicaragua yakata uhusiano wa kidiplomasia na utawala haramu wa Israel
Oct 12, 2024 03:50Serikali Nicaragua imetangaza kuvunja uhusiano wa kidiplomasia na utawala wa Kizayuni wa Israel sambamba na Israel kuendelea na mauaji ya kimbari huko Gaza.
-
Guterres alaani mashambulizi ya Israel dhidi ya walinda Amani wa Umoja wa Mataifa
Oct 11, 2024 23:21Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres siku ya Ijumaa alilaani vikosi vya utawala wa Kizayuni wa Israel vilivyofyatua risasi kwenye kituo cha walinda Amani wa Umoja wa Mataifa nchini Lebanon na kusema uchokozi huo ni ukiukaji wa sheria za kimataifa za kibinadamu.