Mshindi wa Nobel: Hali ya watoto wa Ghaza ni kama ya wa Japan baada ya Vita vya Pili vya Dunia
(last modified 2024-10-14T05:38:51+00:00 )
Oct 14, 2024 05:38 UTC
  • Mshindi wa Nobel: Hali ya watoto wa Ghaza ni kama ya wa Japan baada ya Vita vya Pili vya Dunia

Kundi la Nihon Hidankyo, mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel ya 2024 limesema, hali ya watoto katika Ukanda wa Ghaza ni sawa na hali ya watoto wa Japan ilivyokuwa mwishoni mwa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.

Kundi la Nihon Hidankyo, lililoasisiwa mwaka 1956 na manusura wa mashambulio ya mabomu ya atomiki yaliyofanywa na jeshi la Marekani dhidi ya miji ya Japan ya Hiroshima na Nagasaki, limeshinda Tuzo ya Amani ya Nobel kwa jitihada zake za kupigania kuwepo ulimwengu usio na silaha za nyuklia na kubainisha hatari ya utumiaji wa silaha hizo.
 
Tomoyuki Mimaki, Mwenyekiti Mwenza wa kundi hilo amesema, hali ya watoto huko Ghaza ni sawa na hali ya watoto wa Japan ilivyokuwa miaka 80 iliyopita.
Tomoyuki Mimaki

Akiongea huku akibubujikwa na machozi Mimaki ameeleza kuwa watoto huko Ghaza wanafunikwa na damu na kuishi kila siku bila ya chakula na akaongezea kwa kusema, hakuwahi kufikiria kama kitu kama hicho kingetokea kwa wanadamu.

 
Ofisi ya Habari ya Serikali ya Palestina katika Ukanda wa Ghaza imetangaza kuwa karibu watoto 17,000 wameuawa shahidi tangu vilipoanza dhidi ya eneo hilo mnamo Oktoba 7, 2023.../

 

Tags