-
Data za Waindonesia milioni sita akiwemo Rais na wanawe zavujishwa na kuuzwa tovutini
Sep 20, 2024 03:21Data za walipakodi milioni sita katika taifa la nne kwa idadi kubwa zaidi ya watu duniani, Indonesia, zikiwemo za Rais anayemaliza muda wake Joko Widodo, zimedaiwa kuvujishwa na kuuzwa. Hayo ni kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na vyombo vya habari jana Alkhamisi.
-
Maafisa wa US hawaamini kama vita vitaweza kusimamishwa Ghaza wakati wa urais wa Biden
Sep 19, 2024 23:50Maafisa kadhaa wa serikali ya Marekani wameliambia gazeti la Wall Stree Journal kwamba hawaamini kama makubaliano ya kusitisha vita kati ya utawala wa Kizayuni wa Israel na harakati ya Hamas huko Ghaza yataweza kufikiwa kabla ya Rais Joe Biden kuondoka madarakani mwezi Januari.
-
Onyo la UN kuhusu matumizi mabaya ya zana za kiraia kwa madhumuni ya kigaidi
Sep 19, 2024 23:00Kufuatia wimbi kubwa la milipuko ya kigaidi nchini Lebanon ambayo imelenga vifaa vya mawasiliano kama vile pager, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema vifaa vya kiraia havipaswi kugeuzwa kuwa silaha.
-
Viongozi 130 wa dunia kujadili Gaza, Ukraine na Sudan
Sep 19, 2024 09:07Zaidi ya viongozi 130 wa dunia wanatarajiwa kukutana wiki ijayo katika makao mkuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani, kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya migogoro ya kibinaadamu inayoshuhudiwa katika maeneo tofauti ya dunia.
-
Pager zilizotumika katika ugaidi nchini Lebanon 'zilitengenezwa Hungary'
Sep 19, 2024 01:09Kampuni ya Taiwan Gold Apollo inasema kwamba pager zilizotumiwa katika shambulio la kigaidi la Israel dhidi ya Lebanon siku ya Jumanne zilitengenezwa na kampuni ya Hungary.
-
Umoja wa Mataifa waitaka Israel kusitisha kukalia kwa mabavu maeneo ya Wapalestina
Sep 19, 2024 01:05Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio linaloitaka Israel kukomesha uwepo wake kinyume cha sheria katika eneo la Palestina linalokaliwa kwa mabavu ndani ya mwaka mmoja.
-
WHO: Vifaru vya Israel vinawashambulia wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu
Sep 18, 2024 07:56Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa vifaru vya wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel vimewashambulia wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu huko kaskazini mwa Ukanda wa Gaza ili kuwazuia kutoa misaada kwa wakimbizi na majeruhi wa Kipalestina.
-
Kampuni ya Taiwan yakanusha kutengeneza vifaa vya mawasiliano vilivyoripuka Lebanon
Sep 18, 2024 04:25Kampuni ya Gold Apollo ya Taiwan imekanusha kuwa ndiyo iliyotengeneza vifaa vya mawasiliano vya 'Pagers' vilivyoripuka nchini Lebanon.
-
Msaada wa EU kwa Ukraine tangu vilipoanza vita na Russia 2022 umefikia dola bilioni 131
Sep 18, 2024 02:32Misaada iliyotolewa na Umoja wa Ulaya (EU) na nchi wanachama wa umoja huo kwa Ukraine tangu vilipoanza kati ya nchi hiyo na Russia mnamo Februari 2022 imefikia yuro bilioni 118 (dola bilioni 131). Hayo yameelezwa na Makamu wa Rais wa Tume ya EU Valdis Dombrovskis.
-
Vizingiti vya washirika wa uhalifu wa Netanyahu katika kutolewa hukumu katika mahakama ya ICC
Sep 17, 2024 22:50Katika hali ambayo, wasiwasi wa duru za Kizayuni kuhusiana na utoaji wa hati za kukamatwa na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai dhidi ya Netanyahu na Gallant kwa tuhuma za kufanya jinai za kivita, Mwanasheria Mkuu wa mahakama hii amefichua kuwa wakuu wa baadhi ya nchi wamemshinikiza asitoe waranti wa kutiwa mbaroni Gallant na Netanyahu.