Vizingiti vya washirika wa uhalifu wa Netanyahu katika kutolewa hukumu katika mahakama ya ICC
Katika hali ambayo, wasiwasi wa duru za Kizayuni kuhusiana na utoaji wa hati za kukamatwa na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai dhidi ya Netanyahu na Gallant kwa tuhuma za kufanya jinai za kivita, Mwanasheria Mkuu wa mahakama hii amefichua kuwa wakuu wa baadhi ya nchi wamemshinikiza asitoe waranti wa kutiwa mbaroni Gallant na Netanyahu.
Karim Khan, Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) amefichua mashinikizo yaliyoenea ya wakuu wa baadhi ya nchi dhidi yake ili uachane na uamuzi wa kutoa hati za kukamatwa Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu na Waziri wa Vita wa Utawala wa Kizayuni Yoav Gallant na kusisitiza kwamba, baada ya kupata habari kuhusu ushahidi wa kutoa hati za kukamatwa kwa Netanyahu na Galant na kusisitiza kwamba, binafsi anaona kukamatwa kwao ni muhimu na jambo la dharura ili kuzuia kuendelea kwa uhalifu kwa mujibu wa Mkataba wa Roma.
Utawala wa Kizayuni unashauriana na zaidi ya nchi 120 wakiwemo washirika wake wote wa Magharibi, ili kubatilisha utolewaji wa hati ya kukamatwa na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai na kufuta uwezekano wa kukamatwa wanasiasa wake katika ardhi yao ili wakabidhiwe kwa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai.
Kuhusiana na hilo, Waziri wa Sheria wa utawala wa Kizayuni, Yariv Levin, kwa ombi la Netanyahu, amemtaka Gali Baharav Miara, mshauri wa mahakama wa baraza la mawaziri kufungua kesi ya jinai kuhusiana na vita vya Gaza dhidi Gallat na Netanyahu ili kuweka pembeni ombi la Mahakama ya Kimataifa ya Jinai la kutoa hati za kukamatwa kwao.
Kanali ya 12 ya Televisheni ya utawala wa Kizayuni imebainisha kuwa, Netanyahu anakusudia kufungua faili hili na kulifunga katika siku zijazo na hivyo kutangaza kuwa, utawala wa Kizayuni umechunguza tuhuma za vita dhidi ya mawaziri hao na hivyo hakuna haja kwa mahakama hiyo kuingilia kati.
Lakini Baharav Miara alipinga ombi hili na akaliona kuwa ni "janja ya wazi" ambayo haitaweza kuzuia Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) kuendelea na uchunguzi wake, lakini kwa hili, ni muhimu kuunda kamati ya juu ya kutafuta ukweli ili kuchunguza shambulio la Oktoba 7 la Hamas na Vita vilivyofuata dhidi ya Ukanda wa Gaza.
Kuhusiana na hili, Karim Khan ameitaka Tawi la Kwanza la Mahakama ya Kimataifa ya Jinai kutoa "haraka iwezekanavyo"; hati za kukamatwa zilizoombwa dhidi ya Netanyahu na Gallant; kwa sababu hati hizi za kukamatwa ni muhimu kwa sababu ya "uhalifu usiokoma" uliotajwa katika ombi la awali na "hali ya Palestina ni mbaya," na mwendesha mashtaka mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu anaona kuwa, mahakama hiyo inafuatilia kesi iliyotajwa kutokana na majukumu iliyonayo ya kuchunguza makosa manne ya kimataifa ikiwa ni pamoja na vita, uhalifu, uhalifu dhidi ya ubinadamu, mauaji ya halaiki na uhalifu wa ubakaji.
Kwa ombi la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa au mojawapo ya nchi 124 wanachama wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai, mwendesha mashtaka anaweza kuanzisha uchunguzi; kama ambavyo mwendesha mashtaka wa mahakama anaweza kuanzisha uchunguzi kwa ubunifu wake wenyewe, kama ilivyotokea katika faili la kesi ya Palestina.
Fatou Bensouda, mtangulizi wa Karim Khan, alianzisha uchunguzi dhidi ya utawala wa Kizayuni mwaka 2021, ambao ulikuwa msingi wa uchunguzi wa Karim Khan. Marekani ikiwa ni mshirika mkuu wa utawala wa Kizayuni katika kutenda jinai za kivita huko Gaza, inadai kuwa mwendesha mashtaka mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai anapaswa kuanzisha uchunguzi mpya ili kusiwe na wasiwasi wowote kuhusu mchakato huo wa kisheria.
Kadhalika, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Anthony Blinken anadai kuwa, mwendesha mashtaka ana haraka ya kutoa hati za kukamatwa kwa maafisa wa utawala wa Kizayuni, na hilo halitoi fursa kamili kwa mamlaka ya Kizayuni na mfumo wake wa kisheria kukusanya nyaraka na ushahidi.
Marekani na utawala wa Kizayuni si wanachama wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) na hawajatia saini Mkataba wa Roma. Ujerumani pia imetoa madai sawa na hayo na kusema: Kwa kuwa Israel kwa sasa iko vitani, hivyo ilipaswa kupewa fursa ifaayo na halisi ya kuandaa ushahidi na majibu ya tuhuma hizo.
Madai na vizuizi hivyo vinatolewa huku utawala wa Kizayuni ukifanya mashambulizi ambayo hayajawahi kushuhudiwa dhidi ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na wakati huo huo ukiendelea na mashambulizi yake ya jinai huko Gaza. Kwa mujibu wa wataalamu, hatua hiyo ni natija ya jamii ya kimataifa kutojali na kunyamazia kimya jinai zilizofanywa na utawala huo dhidi ya Gaza katika kipindi cha miezi kadhaa iliyopita. Ukweli wa mambo ni kuwa, nchi za Magharibi kwa kukwamisha njia ya kutolewa hati na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai dhidi ya Waziri Mkuu na Waziri wa Vita wa Israel, zinaandaa uwanja na mazingira ya kutenda jinai zaidi.
Miongoni mwa mambo mengine ni kuwa, kutolewa kwa hukumu hiyo katia hatua ya awali kutamaanisha kutambuliwa kwa jinai za kivita na dhidi ya binadamu za viongozi wa Kizayuni na wauungaji mkono wake wanaotoa msaada wa silaha kwa utawala huo, uamuzi ambao pengine utapelekea kuongezeka kutengwa kisiasa na kuwekewa vikwazo, Waziri Mkuu na Waziri wa Vita wa utawala wa Kizayuni na hivyo kutoweza kusafiri katika nchi wanachama 124 wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai.
Kwa sababu nchi hizi zitazimika kuwaweka kizuizini, na tatu ni kuwa mgogoro wa kiuchumi wa utawala wa Kizayuni utaongezeka baada ya vita vya Gaza.