Askari 20 wa Kizayuni waaangamizwa katika muda wa mwezi mmoja pekee
(last modified Thu, 03 Jul 2025 04:30:01 GMT )
Jul 03, 2025 04:30 UTC
  • Askari 20 wa Kizayuni waaangamizwa katika muda wa mwezi mmoja pekee

Gazeti la Kizayuni la Yediot Aharonot limeandika katika ripoti yake kuwa: Mwezi uliopita wa Juni Israel imeshuhudiwa kuawa idadi kubwa ya wanajeshi wake huko Gaza mwaka huu.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, mwezi uliopita wa Juni wanajeshi 20 wa Kizayuni waliangamizwa; 15 kati yao waliuawa tarehe 24 Juni katika mapigano huko Khan Yunis kusini mwa Gaza. 

Hivi karibuni wanamuqawama wa al Qassam waliwaangamiza wanajeshi watatu wa Kizayuni kwa kutumia silaha nyepesi mashariki mwa mji wa Jabaliya kaskazini mwa Ukanda wa Gaza. 

Tawi la kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) baada ya kurejea katika mstari wa mapambano lilitangaza kuwa limewauwa kwa karibu wanajeshi watatu wa Kizayuni kwa kutumia silaha nyepesi huko mashariki mwa mji wa Jabaliya unaopatikana kaskazini mwa Ukanda wa Gaza. 

Utawala wa Kizayuni tangu Oktoba 7 2023 ulianzisha vita na mauaji ya kimbari dhidi ya wakazi wa Gaza kwa malengo mawili makuu mawili yaani kuliangamiza kundi la Hamas na kuwarejesha mateka wao wa Kizayuni hata hivyo Israel imeshindwa kufikia malengo hayo iliyoyataja na kulazimika kufikia mapatano na Hamas ili kubadilishana mateka.