Hizbullah: Wavamizi wa Quds hawatakuwa na nafasi kusini mwa Lebanon
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i127830-hizbullah_wavamizi_wa_quds_hawatakuwa_na_nafasi_kusini_mwa_lebanon
Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema: Utawala wa Kizayuni wa Israel hauwezi kuwa na nafasi katika ardhi za kusini mwa Lebanon.
(last modified 2025-10-16T03:06:03+00:00 )
Jul 02, 2025 02:11 UTC
  • Sheikh Naim Qassim
    Sheikh Naim Qassim

Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema: Utawala wa Kizayuni wa Israel hauwezi kuwa na nafasi katika ardhi za kusini mwa Lebanon.

Sheikh Naim Qassim amesema, muqawama hauruhusu wavamizi kuweko katika eneo hilo.

Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon, amebainisha kuwa, katika wakati huu muhimu wa kihistoria, ameyataka baadhi ya makundi kuwa pamoja na Hizbullah ya Lebanon na sio kuwa katika safu ya adui.

Kiongozi huyo wa Hizbullah sambamba na kuwakosoa wale wanaotaka kutoa upendeleo kwa adui, amesitiza: "Sio sisi tunaoipeleka nchi kusikojulikana na hatari, lakini watu waliochagua njia hii ni wale wanaotaka kujisalimisha kwa wavamizi na watu ambao wanakodolea macho ya tamaa ardhi yao."

Sheikh Naim Qassim Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon ameongeza kuwa, "Tuko tayari kuzungumza nanyi kuhusu masuala yote, na kama kuna jambo ambalo linawatia wasiwasi, tutalitatua. Lakini kamwe msiwe upande wa adui."

Aidha amesisitiza kuwa, "Tuko katika nafasi ya kujilinda, tunasimama dhidi ya adui ambaye ni mvamizi na tumesimama kidete kwa ajili ya kukabiliana na  uvamizi wa Marekani na utawala haramu wa Israel."

Kadhalika Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema: "Watu wote ambao ni mabeberu  wanafanya njama kutupotosha, lakini hatuna la kufanya zaidi ya kuelekea katika njia sahihi na kudumisha muqawama."