Viongozi 130 wa dunia kujadili Gaza, Ukraine na Sudan
https://parstoday.ir/sw/news/world-i116544-viongozi_130_wa_dunia_kujadili_gaza_ukraine_na_sudan
Zaidi ya viongozi 130 wa dunia wanatarajiwa kukutana wiki ijayo katika makao mkuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani, kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya migogoro ya kibinaadamu inayoshuhudiwa katika maeneo tofauti ya dunia.
(last modified 2024-09-19T09:07:37+00:00 )
Sep 19, 2024 09:07 UTC
  • Viongozi 130 wa dunia kujadili Gaza, Ukraine na Sudan

Zaidi ya viongozi 130 wa dunia wanatarajiwa kukutana wiki ijayo katika makao mkuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani, kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya migogoro ya kibinaadamu inayoshuhudiwa katika maeneo tofauti ya dunia.

Viongozi hao wataangazia pia masuala ya hali ya hewa pamoja na vita vya Mashariki ya Kati na Ulaya vinavyotishia kutanuka kutokana na kasi ndogo ya juhudi za kuimaliza migogoro hiyo.

Vita vya Gaza, Ukraine na Sudan vitakuwa ndio mgogoro mikuu mitatu itakayopewa kipaumbele katika mkutano huo huku wanadiplomasia na wachambuziwakisema kuwa, hawatarajii maendeleo yoyote kuelekea amani.

Mkutano wa kila mwaka wa viongozi wa dunia huashiria kufunguliwa kwa kikao cha kila mwaka cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na mara nyingi huwa fursa ya kufanyika mikutano ya kidiplomasia.

 

Huku mkutano wa baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ukitarajiwa kufanyika wiki ijayo, walimwengu wameendelea kukosoa utendaji wa Umoja wa Mataifa na Baraza lake la Usalama kutokana na kushindwa kuipatia ufumbuzi migogoro mingi inayoshuhudiwa hivi sasa.

Wachambuzi wa mambo wanasema, Umoja wa Mataifa kimsingi umeshindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo na hivyo kuchangia kuendelea kushuhudiwa migogoro mbalimbali duniani. Aidha undumakuwili wa madola makubwa na hatua yao ya kuutumia Umoja wa Mataifa na Baraza la Usalama kwa ajili ya kufikia malengo yao inatajwa kuwa sababu kuu ya kushindwa kupatiwa ufumbguzi migogoro mingi na vita duniani.