-
White House yakanusha madai kwamba Biden anatibiwa ugonjwa wa Parkinson
Jul 09, 2024 08:22Ikulu ya Rais wa Marekani, White House, imekanusha kuwa Rais Joe Biden wa nchi hiyo anatibiwa ugonjwa wa Parkinson baada ya kitabu cha kumbukumbu za wageni kuonyesha kuwa daktari bingwa wa neva aliitembelea White House mara nane katika miezi ya karibuni.
-
Starmer: Siko tayari kuendeleza mpango wa kuwafukuza wahamiaji na kuwapeleka Rwanda
Jul 07, 2024 08:27Waziri Mkuu mpya wa Uingereza, Keir Starmer, ametangaza kuwa "hayuko tayari" kuendeleza mpango mkuu wa serikali ya awali ya kihafidhina kuwafukuza wahamiaji na kuwapeleka Rwanda.
-
Afisa wa Marekani: Vita vya Hamas huko Gaza vinawahamasisha wengi
Jul 06, 2024 22:51Afisa wa Marekani amesema kuwa, shambulio la Hamas la tarehe 7 Oktoba dhidi ya Israel lilikuwa na litaendelea kuwa tukio la vizazi mbalimbali litakalotumiwa na makundi yenye silaha katika Mashariki ya Kati na duniani kote kama fursa ya kusajili wapiganaji.
-
Gharama za mradi wa makombora ya nyuklia ya US zafikia dola bilioni 160
Jul 06, 2024 07:51Gharama za kufanikisha mradi wa kuzalisha makombora ya nyuklia wa Marekani zimeripotiwa kuongezeka hadi dola bilioni 160.
-
Serikali ya Uingereza yatoa mwito wa kusitishwa haraka vita vya Gaza
Jul 06, 2024 03:19David Lammy, Waziri mpya wa Mashauri ya Kigeni wa Uingereza ametoa wito wa kusitishwa mara moja vita katika Ukanda wa Gaza.
-
Rais wa Marekani alikoroga tena; asema: Naona fahari kuwa mwanamke mweusi
Jul 05, 2024 23:09Rais Joe Biden wa Marekani kwa mara nyingine tena ameboronga katika uzungumzaji na kuonyesha udhaifu wa kiakili, baada ya kudai kuwa yeye ni mwanamke mweusi.
-
Onyo la UN kuhusu ongezeko la vyama vya mrengo wa kulia barani Ulaya
Jul 05, 2024 23:06Volker Turk, Kamishna Mkuu wa Haki za Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa, alionya Jumatano wiki hii kuhusu kuibuka kwa vyama vya mrengo wa kulia vyenye misimamo ya kufurutu mipaka barani Ulaya na kuhatarishwa haki za wahamiaji na wakimbizi.
-
Kukiri kushindwa sera za Biden mkabala wa vita vya Gaza
Jul 05, 2024 10:12Maafisa 12 wa serikali ya Marekani ambao wamejiuzulu nyadhifa zao wakipinga na kulalamikia vita dhidi ya Gaza wamesisitiza katika taarifa yao kuwa sera za Rais Joe Biden wa Marekan mkabala wa Gaza zimefeli, na kutahadharisha kuwa kufeli kisiasa Washington mkabala wa Gaza ni tishio kwa usalama wa taifa wa Marekani.
-
Sunak ainua mikono juu, akiri kushindwa vibaya Chama cha Conservative, Uingereza
Jul 05, 2024 03:59Waziri Mkuu wa Uingereza na kiongozi wa Chama cha Conservative, Rishi Sunak, amekiri kushindwa kwa chama chake katika uchaguzi wa Bunge uliofanyika jana, Alhamisi.
-
Mbunge wa kwanza wa Ujerumani mwenye asili ya Afrika alijiuzulu kutokana na ubaguzi wa rangi
Jul 05, 2024 03:17Mbunge wa kwanza mwenye asili ya Kiafrika katika Bunge la Ujerumani, Karamba Diaby, ametangaza kwamba hatashiriki uchaguzi wa shirikisho mwaka ujao, wiki kadhaa baada ya kufichua jumbe za chuki, zikiwemo za ubaguzi wa rangi na vitisho vya kuuawa, ambazo yeye na wafanyakazi wake wamepokea.