-
Mbunge wa kwanza wa Ujerumani mwenye asili ya Afrika alijiuzulu kutokana na ubaguzi wa rangi
Jul 05, 2024 03:17Mbunge wa kwanza mwenye asili ya Kiafrika katika Bunge la Ujerumani, Karamba Diaby, ametangaza kwamba hatashiriki uchaguzi wa shirikisho mwaka ujao, wiki kadhaa baada ya kufichua jumbe za chuki, zikiwemo za ubaguzi wa rangi na vitisho vya kuuawa, ambazo yeye na wafanyakazi wake wamepokea.
-
Mamilioni ya wananchi wa Uingereza wapiga kura katika uchaguzi mkuu
Jul 04, 2024 08:41Wananchi wa Uingereza Alkhamisi leo wanapiga kura katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kukirejesha madarakani chama kikuu cha upinzani cha Labour, na kumaliza takribani muongo mmoja na nusu wa utawala wa chama cha Conservative.
-
Maafisa wa Marekani waliojiuzulu wakiri kushindwa siasa za Washington kuhusu Gaza
Jul 04, 2024 04:11Maafisa 12 waliojiuzulu wa serikali ya Marekani wamekiri kushindwa siasa za Rais Joe Biden wa Marekani kuhusu Ukanda wa Gaza.
-
Muendelezo wa maandamano dhidi ya Wazayuni katika maeneo mbalimbali ulimwenguni
Jul 04, 2024 03:40Maandamano bado yanaendelea katika nchi tofauti za dunia kupinga mauaji ya halaiki yanayofanywa na jeshi katili la utawala wa Kizayuni huko Ukanda wa Gaza.
-
Putin asifu uhusiano unaokua kwa kasi kati ya Russia na Uturuki
Jul 03, 2024 22:55Rais Vladimir Putin wa Russia amesema kuwa uhusiano kati ya nchi yake na Uturuki unakuwa kwa kasi licha ya changamoto zilizopo za kimataifa.
-
Russia: Zaidi ya wanajeshi 1,900 wa Ukraine wameuawa katika masaa 24
Jul 02, 2024 23:19Wizara ya Ulinzi ya Russia imetangaza kuwa wanajeshi 1,940 wa Ukraine wameuawa katika muda wa saa 24 huku jeshi la Russia likiendelea kupata nguvu na kusonga mbele zaidi.
-
Amnesty International: Wanaharakati 3 kati ya 5 wa haki za binadamu wanakabiliwa na unyanyasaji
Jul 02, 2024 23:19Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limesema kuwa wanaharakati 3 kati ya 5 vijana wanakabiliwa na unyanyasaji mtandaoni duniani kote kwa kuchapisha maudhui inayohusiana na haki za binadamu.
-
Lavrov kuendesha mjadala wa Baraza la Usalama kuhusu Mashariki ya Kati
Jul 02, 2024 09:03Russia ambayo inashikilia uwenyekiti wa kiduri wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa mwezi huu wa Julai imetangaza kuwa Waziri wake wa Mambo ya Nje Sergei Lavrov ndiye atakayesimamia vikao kadhaa vya mikutano ya baraza hilo mwezi huu, ikiwa ni pamoja na mjadala kuhusu hali ya mambo ya Mashariki ya Kati.
-
Bendera za Israel, US zachomwa moto Brazil katika maandamano ya kuiunga mkono Palestina
Jul 02, 2024 02:42Wananchi wenye hasira wa Brazil wamechoma moto bendera za Israel, Marekani na Umoja wa Ulaya wakati wa maandamano ya kuunga mkono Palestina na kupinga mauaji ya kimbari yanayoendelea kufanywa na utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza.
-
Chama tawala Australia chamwadhibu mbunge wa kike anayevaa hijabu kwa kuunga mkono dola huru la Palestina
Jul 02, 2024 00:40Chama tawala cha Labour nchini Australia kimeamua kumfukuza mwakilishi Fatima Byman kutoka kwenye kundi lake la Baraza la Seneti kwa muda usiojulikana kwa sababu ameunga mkono pendekezo la Chama cha Kijani la kutambua rasmi Palestina kama taifa huru.